Pages

Friday, February 1, 2013

WAKILI WA LULU ASIKITISHWA NA WASANII WA FILAMU KUTOKUWA NA USHIRIKIANO

Siku chache baada ya kuachiwa kwa dhamana kwa kesi inayomkabili ya kudaiwa kuua bila kukusudia actress Elizabeth Michael(Lulu).Wakili wake Peter Kibatala amesema kuwa amesikitishwa na kitendo cha wasanii wa tasnia hiyo kushindwa kujitokeza mahakamani siku zote kesi hiyo ikiwa inaendelea na hata siku ya mwisho wakati Lulu anapewa dhamana walishindwa kuwepo na kutoa ushirikiano wa kutosha kumfariji mwenzao. Wakili huyo akizungumza na vyombo vya habari alisema kuwa kitendo cha wasanii hao kutojitokeza mahakamani siku zote za kesi au siku ya mwisho ambayo Lulu alikuwa anapewa dhamana kunatia shaka kuwa ndani ya tasnia hiyo hakuna upendo wa kweli na huwa wanapendana kwenye raha pekee. Mbali na hayo wakili huyo amewapongeza Dr. Cheni na Monalisa kwa kuonyesha upendo wa dhati kwa muigizaji mwenzao kwa kuwa bega kwa bega na familia ya Lulu hadi siku ya mwisho anapewa dhamana ndiyo waliompokea .Baadhi ya wasanii walipoulizwa juu ya kutoonekana mahakamani walisema walikuwa busy na kazi na siku ambayo msanii huyo anapata dhamana walikuwa kambini na sehemu nyingine ambazo ni vigumu wao kutoka.
Yvon Cheryl(Monalisa)

No comments:

Post a Comment