Wednesday, February 20, 2013

PLEASE ! ACTORS WA TANZANIA SHUGHULIKIENI TATIZO HILI HARAKA.

Hili tatizo nimeliona muda mrefu sana hasa ninapoangalia films za kitanzania lakini mpaka sasa hakuna juhudi zozote zinazoonekana kuchukuliwa ili kuliondoa na tayari limeanza kuathiri baadhi ya wasanii tena bila wao kujua. Ni hivi ni kwanini majina ya actors wengi wa kitanzania huwa hayaeleweki yaani hakuna jina maalum la kumtambulisha muigizaji iwe magazetini au katika makava ya films na films zenyewe unakuta msanii mmoja anaitwa majina mbalimbali au film 1 lakini jina la msanii limeandika tofauti zaidi ya mara mbili au tatu?. mfano katika film fulani actress ameandikwa kama Sabrina Rupia juu ya kava la film, katika poster la film hiyo hiyo ameandikwa Ketty Rupia ndani ya films Ameandikwa Cathy Rupia au film moja na nyingine jina la msanii mmoja limeandikwa tofauti kabisa. Angalia mifano hii zaidi jinsi majina ya wasanii yanavyoandikwa Slim

Omar/Slim Mrisho, Jack wa Chuzi/Jackline Pentezel, Jini Kabula/Miriam Jolwa, Nora/Nuru Nasoro, Yobnesh/Yobnesh Yussuph/Batuli,Tino/Hisan Muya/Tino Muya, Cloud/Issa Mussa/ 112 Cloud na wengineo kibao. Wapo wengine ambao siyo waigizaji but majina yao pia yanatokea tofauti tofauti. Naomba niseme wazi kuwa tatizo hili kwa kiasi kikubwa limechangiwa na magazeti ya udaku kwa kuwapachika wasanii majina ya uhusika wao katika michezo ya kuigiza/films au majina ya wapenzi wao bila hata idhini ya wasaii wenyewe. Matokeo yake baadhi ya majina hayo yamekuwa maarufu kwa kuandikwa sana magazetini hata kama msanii husika halitaki jina hilo. Mfano Muigizaji Nuru Nassoro aliwahi kusema wazi kuwa hataki kuitwa Nora bali aitwe jina lake halisi....endelea chini

Wito wangu ni kuwa wasanii wajitokeze sasa na kusema majina yao wanayotaka kujulikana kisanii maana hii imesababisha wengine hata kukosa followers katika mitandao ya kijamii hasa wanapotumia majina yao halisi ambayo hayajulikani. Hii haitakiwi kwa msanii mmoja mmoja bali wasanii wote ambao wana tatizo hili wanaweza kufanya press conference na wakawaeleza kila kitu waandishi wa habari kwa kuwa hawa hawa ndio wamesababisha hivyo wanaweza kutatua tatizo. Jina la kutumia ni sehemu ya malengo ya msanii katika kazi zake so kama msanii anaitwa na kuandikwa majina kibao si anachanganya mashabiki wake na hata kushindwa kuwaweka pamoja. Pia tatizo hili waambiwe film editors na graphic designers kwa kuwa wao pia wamelisababisha kwa kiasi kikubwa. lakini ili hili lifanikiwe waigizaji wenyewe wanatakiwa walitatue mapema la sivyo litazidi kuja kuwaathiri zaidi hata huko mbeleni na hata kimataifa licha ya kuonekana dogo

kwa sasa. Mfano muigizaji Ramsey Hashimu huko Ghana ameandikwa Ramsey Hashimu but media za Tanzania zinamuandika Hashim Kambi wakati yeye mwenyewe facebook anatumia Ramsey Hashim, sasa kama huku si kukosa msimamo ni nini! Mtu huyu anaweza kuwakusanya mashabiki wake pamoja kweli ! media badilikeni na wasanii shughulikieni hili tatizo. mapema. Pia ushauri wangu wa mwisho kuna wasanii wengi wana majina ya kawaida sana hivyo kukosa mvuto hasa katika safari zao kuelekea soko la kimataifa, mfano watumie majina yao ya ukoo na siyo ya baba zao maana mengi ni common sana but ya ukoo hayana watu wengi, wengine si lazima utumie majina mawili bali jina moja linaweza kukuweka na kukutambulisha kimataifa bila tatizo. mfano Shilole litumike badala ya Zuwena Mohamed, Yobnesh litumike badala ya Yobnesh Yusuph au Batuli.
Wasanii pia acheni kasumba na ushamba wa kujipachika majina kila kukicha inaonyesha hamna malengo na sanaa bali kuuza sura kupitia majina.

                                                  
                                                   AHSANTENI


No comments:

Post a Comment