Monday, January 28, 2013

LULU HAJAACHIWA BADO, DR. CHENI KUTOA MILIONI 2O KWA AJILI YA DHAMANA YAKE !

Lulu hajaachiwa, atarudishwa mahakamani kesho kwakuwa Msajili wa Mahakama Kuu hakuwepo na hii ilikuwa ni kesi ya Kuua bila kukusudia. Kesho wadhamini watawasilisha nyaraka zao mbele ya msajili ndipo anaweza kuachiwa ,hii ni kwa mujibu wa JAMIIFORUM.Kwa upande mwingine mwigizaji Muhsin Awadhi au Dr. Cheni amesema yupo tayari kuwa mmoja wa wadhamini wa muigizaji mwenzake Lulu ambaye anakabiliwa na kesi ya kuua bila kukusudia katika kifo cha muigizaji Steven Kanumba. Akiongea na clouds fm katika mahakama kuu ya Tanzania leo hii ambapo lulu alipewa nafasi ya dhamana yake Dr. Cheni alisema masharti yote ya dhamana hiyo yanatekelezeka "kwa mfano wamesema kuna dhamana ya milioni 20 na mtu mwingine milioni 20 mimi naweza nikajitoa katika mmojawapo katika upande huo", aliendelea "masharti mengine sidhani kama ni magumu kwasababu kila kitu kiko okay sidhani kama kitashindikana sasa hatujajua msajili atakapopata anatoa leo ama atamtoa lini sababu na yeye lazima apate muda wa kupitia yawezekana ana mafaili mengi juu ya meza". Tangu kukutwa na masahibu hayo Dr. Cheni amekuwa bega kwa bega na familia ya Lulu katika kufuatilia kesi, kutafuta mawakili na mengineyo na inasemekana Dr. Cheni ndiye aligundua kipaji cha Lulu na kumpeleka kaole. sisi tunampongeza Dr. cheni kwa kuwa na moyo wa kibinadamu kwa kuwa bega kwa bega na msanii mwenzake katika kipindi hiki cha matatizo.

No comments:

Post a Comment