Wednesday, December 26, 2012

COLETHA RAYMOND: HAKUNA WA KUNITISHA SWAHILIWOOD

Filamu za kitanzania zinazidi kujizolea umaarufu mkubwa afrika mashariki na barani afrika kwa ujmla kila uchao, swahiliwood imejaaliwa waigizaji wenye sifa mbalimbali na tofauti na mmoja wao akiwa ni muigizaji maarufu wa kike Coletha Raymond. Muigizaji huyu amejaaliwa kipaji cha uigizaji hilo halina shaka, uzuri wa sura na umbo linaloweza kumtoa Obama white house Marekani na kuja bongo kumuona this bombshell actress. Nilibahatika kupata chance ya kumuuliza Coletha mawili matatu hivyo sikumchelewesha nikamnyuka maswali ya maana.
SWALI:Unapoletewa script ya filamu nini kinakuvutia mpaka kukubali kucheza filamu husika, yaani uzuri wa script,co-stars au director ndiyo hukuvutia?
COLETHA: Kibongobongo pesa tu.......lakini toka moyoni napenda hadithi ikiwa nzuri na script itulie.
SWALI:Ni muigizaji gani wa swahiliwood ambaye anakuvutia sana kikazi hujawahi kufanya nae kazi pamoja na ungependa kufanya nae filamu pamoja?
COLETHA:Wema Sepetu, japo nimecheza nae kwenye film ya Dj Ben lakini sikukutana nae kwenye scene yoyote.
SWALI:Kati ya Bongomovie na TAFF kipi ni chombo ambacho kwa mtazamo wako kina malengo ya kuipaaisha sanaa ya filamu Tanzania?
COLETHA:Mhhh....huu ni mtihani! vyote
SWALI:Unafikiri taswira halisi ya mwanamke wa kitanzania inaonyeshwa katika filamu zetu au ni uigaji wa maisha ya kigeni zaidi?
COLETHA:Mengi tufanyayo ni maisha ya kigeni lakini ndo maisha halisi because kila kitu tunaiga kutoka kwa wenzetu.
SWALI:Ni muigizaji gani wa kike Tanzania anakupa homa ya jiji hasa kutokana na kazi zake kuwa za kiwango cha hali ya juu?. Unao mpango wa kuwa director na producer kama wengine na mashabiki wako watarajie nini kutoka kwako mwaka ujao?
COLETHA:Mhhhh....bado sijaona wa kunipa homa ya jiji kwa kweli ila wanajitahidi. Ahh...mimi sijasomea u-director so siwezi labda kuwa producer... mambo yanakuja wewe subiri ndo najipanga mwanawaneeeee.

No comments:

Post a Comment