Saturday, December 20, 2014

Steps Mmenichefua Sana, Hivi Mnajua Tulivyohangaika Na Hii Sanaa?: Monalisa

Monalisa
Monalisa Yvonne Cherryl mmoja wa waigizaji maarufu ambao wamepigana sana kuifikisha tasnia ya filamu Tanzania hapa ilipo leo ameonekana kutoridhishwa na hatua walioichukua kampuni ya Steps Entertainment kuuza filamu za kitanzania kwa shilingi 1500 badala ya 3000 kwa bei ya rejareja kuanzia mwakani mwezi wa pili.

Hatua hiyo imepingwa na wasanii wenye msimamo mkali kutaka usawa na haki kwa wasanii wote kufaidika na kazi zao ili kuzidi kuikuza sanaa ya filamu nchini, kutafuta mbinu mbadala za kuondoa uharamia ikiwemo kuzidi kuishinikiza serikali itilie mkazo katika sanaa na sio hatua iliyochukuliwa na Steps kwa madai kuzidi kushusha bei ya filamu za nyumbani ni kuzidi kuiua tasnia kwa kuwaondoa wasambazaji wengine sokoni.

Katika kuunga hoja ya Mtitu Monalisa mmoja wa waigizaji wanaoheshimika sana nchini aliandika
"Yaani mi nimechefuka hatari...hivi jamani wanajua tulivyohangaika na hii sanaa hadi hapa tulipofika?1500? kweli? kwa style hii kiwanda chetu kitakuwa kweli? @williammtitu"

 Steps ambayo kwa muda mrefu inalaumiwa kuzifanyia kujuma kampuni nyingine ili ziondoke katika soko ibaki peke yake imedai imefikia hatua hiyo ili kupambana na uharamia. Lakini wasambazaji wengine na wasanii wasio chini ya kampuni hiyo wanaamini ni hujuma za kutaka kuendelea kuwatawala hata wale amabo wamejinasua na kuanza kusambaza kazi zao wenyewe mmoja wapo aliyekemea uamuzi huo akiwa ni William Mtitu msanii maarufu, producer wa siku nyingi na sasa msambazaji ambaye kwa muda sasa amekuwa wazi kusema kampuni hiyo inayomilikiwa na raia wa Tanzania wenye asili ya kihindi wanawanyonya wasanii kimapato, huku wasanii wengine wakilalamikia hilo kimya kimya.
  
Katika mkutano na waandishi wa habari jana wakati Steps Entertainment ikitangaza uamuzi huo baadhi ya wasanii ambao walikuwepo kuungana na Steps ni JB. King Majuto, Niva Zubery, Rammy Galis.

Wasanii katika mkutano na waandishi wa habari jana

No comments:

Post a Comment