Kampuni ya Haak Neel Production na Filamucentral waandaaji wa Tamasha la Dar Filamu Festival wanawakaribisha watengenezaji wote wa filamu zinazotumia Lugha ya Kiswahili kutuma au kuwakilisha filamu zao katika ofisi za Haak Neel Production zilizopo Mikocheni kwa Mwalimu Nyerere.
Tamasha kubwa kabisa la filamu Swahiliwood hilo linapokea kazi zilizotoka mwaka 2013/2014 kwa ajili ya kuonyeshwa katika tamasha kubwa linalounganisha wadau na watengeneza filamu kutoka sehemu mbalimbali za Ulimwengu na kutoa fursa kwa wadau wengi kutengeneza soko lingine.
Akiongea na FC mkurugenzi wa Haak Neel Production Godfrey Katula amesema kuwa tamasha la mwaka huu litakuwa la aina yake kwani litafika kila kona ya Wilaya za Dar es Salaam na kutoa burudani ya kazi nzuri zinazotengenezwa na watanzania.
“Kama ilivyo kauli mbiu yetu inasema “FILAMU ZETU, MAISHA YETU” ni kauli mbiu ya kutia matumaini kwa watengenezaji na watazamaji kwani filamu tuaamini kuwa ni kazi inayoweza kutengeneza ajira kubwa kwa kila mtu,”anasema Katula.
Tamasha hili ambalo limelenga kukuza Lugha ya Kiswahili na kufanya kuwa ni biashara na alama kubwa kwa filamu zetu zinateka soko Afrika ya Mashariki kwa kuongea Kiswahili kitamu na kinzuri kinachovutia kwa wanaAfrika mashariki na Ulaya.
Mtengenezaji wa filamu au mtayarishaji unatakiwa kuwakilisha filamu nakala mbili za filamu ambayo imetoka mwaka na kuonyeshwa kwa mwaka 2014, ikiwa samba na utambuzi wa mtayarishaji, imekaguliwa na Bodi ya Filamu pamoja na taratibu husika katika taasisi za filamu.
Kwa mawasiliano na jinsi ya kuwakilisha filamu zenu wasiliana na +2552773113, +255754 578 730, +255754 260 688 Ongea na Dada Unce anakupatia maelekezo ya kufika katika ofisi za Haak Nell Production.
No comments:
Post a Comment