Pages

Friday, October 24, 2014

Matokeo Halisi Miss Tanzania 2014 Sitti Mtemvu Adaiwa Kushika No.3 Jihan No.1, Majaji Wadai Yalichakachuliwa Jukwaani.

Jihan, Sitti Mtemvu na Lilian Kamazima
Mapya kuhusu Miss Tanzania 2014 yanazidi kuibuka huku issue ya umri wake ikiendelea kuchunguzwa na mamlaka husika.
Habari mpya ni kuwa kwa mujibu wa baadhi ya majaji wa Miss Tanzania mwaka huu matokeo halisi ni kuwa Sitti Mtemvu alishika nafasi ya 3 huku huku Jihan Dimachk akiwa ndiye mshindi wa Miss Tanzania. Majaji hao wanaodaiwa kuanza kuvujisha issue hiyo wanadai kuwa matokeo yalichakachuliwa juu ya jukwaa na hata wao walishangaa.

Vilevile Lemutuz mmoja wa watu wanaodaiwa kuhusika katika uandaaji wa Miss Ilala pia amekuwa akilalamikia kitendo hicho katika mitandao ya kijamii na kudai matokeo halisi yalichakachuliwa kwa mujibu wa taarifa alizopewa na baadhi ya majaji. Lemutz msimamo wake ni kuwa Jihan ndiye mshindi halali wa Miss Tanzania 2014 ambapo watanzania wengi wameonyesha kumkubali na kudai ameonewa.

No comments:

Post a Comment