Thursday, October 23, 2014

Lucy Komba Awachana Kwa Kirefu Mahasidi Wa Ndoa Yake.

Moja ya gauni alilovaa Lucy kwenye ndoa yake
Wiki chache nyuma star wa filamu nchinialifunga ndoa na mpenzi wake mzungu wa siku nyingi ambaye ni raia wa Denmark. Hata hivyo kama ilivyo ada baadhi ya watu hawakuacha maneno maneno kuhusu harusi ya Lucy huku wakidai gauni alilovaa halikuwa zuri kuendana na hadhi yake kama msanii maarufu.
Swahiliworldplanet ililazimika kumtafuta Lucy ambaye pia alionekana kuchoshwa na maneno maneno hayo ambayo mengine yanadaiwa kutoka kwa baadhi ya wasanii wenzake. Hicho hapo chini ndicho alichokisema Lucy ambaye pia filamu yake mpya inayoitwa Kwanini Nisimuoe akiwa na Hamad Ndikumana inatarajiwa kuingia sokoni siku chache zijazo......

"Nilikaa kimya kwanza nikifaidi utamu wa ndoa sasa nimeona nitoe yangu ya moyoni, inaonekana kila mtu alitamani nafasi niliyoipata mimi ya kufunga ndoa, kwanini watu wengi iliwauma? Marafiki, wasanii nk wengi hawakufurahia Lucy kufunga ndoa, kwani walifikiri Lucy ni mwanaume kwamba hatakaa apate mwenza wa maisha yake? Napata jibu kwamba Lucy ninaogopewa kwa kila idara, wapo waliosema Lucy mbaya hana sura ya usanii? Kwani sura ya usanii ikoje? Wasanii wote wakiwa wazuri wabaya wasipate nafasi za kucheza?

 Saa imeingiliwa, Wapo waliosema Lucy hataolewa tutaona, na baada ya kuona Lucy anakaribia kuolewa wakasema mwanaume mwenyewe mzee, na walipoona ndoa imefungwa wakaanza loh hajui kuvaa nguo ya kipaimara aliyovaa bibi yetu miaka ya 40 mara yuko natural hajapambwa sana, kwani nguo ya kipaimara imenifanya ndoa isifungwe? Au padri alisema ukivaa nguo ya kipaimara huwezi kupata ndoa?

 Hapana kwani make up ndiyo nini? Inazuia nini mtu kufunga ndoa, kwani bila make up ndoa haitabarikiwa? Kwa upande wa make up mimi mwenyewe siyo mpenzi kwa hiyo kwa suala hilo mtu asiniingilie, mimi bila make up napendeza na sipendi make up, hasa make up za siku hizi wasichana wanajipamba mpaka sura inabadilika wanakuwa kama uso wameufanyia plastic surgery nani kasema, hapana siyo Lucy mimi, au mnafikiri ng'ombe ukimnyonyoa manyoa atabadilika kuwa mbuzi? La hasha atabaki kuwa ng'ombe.

 Watu waliniponda sana kwenye ndoa yangu lakini baada ya ndoa kuisha wapo waliokaa makundi wakaanza kunichambua mara oh mzungu mwenyewe mvuta bangi mara oh mzungu mwenyewe hana hela, nani alikaa na mume wangu akamwambia hana hela? Na nani kasema mapenzi ni pesa, au nani kasema kila anayeolewa na mzungu anafuata pesa,  au nani kapanga kila msanii aolewe na mtu mwenye pesa, si ndiyo maana mnafuata pesa mnaonjwa onjwa na kuachwa, mara oh Lucy mwenyewe hajampenda mume wake, jamani nani nilishakaa nae nikamwambia mume wangu sijampenda?

 Majungu too much wasanii, naombeni watu waniache na maisha yangu sipendi majungu wala sipendi kugombana na watu, kwenye maisha yangu binafsi, mniingilie, kwenye maisha ya kazi zangu mniingilie, au mmeshtuka sana kusikia Lucy anaolewa na hakuwa mtu wa kujishaua? Kwanini wasanii hatupendani? Kwanini kama unaona mtu kakuzidi usikae nae chini umuombe ushauri nae akusaidie? Mnafikiri tukijishusha tutakuwa tumejidhalilisha?

Sitaki wanafiki yule aliyeona kaingizwa kwenye sanaa na mimi kimakosa basi na ajirudishe nyuma aanze upya aingizwe na mtu anayeona anamfaa kumuingiza kwenye sanaa. I don't care. Yule anayeona mimi ni mtu muhimu kwake aendelee kuona  hivyo. Wapo ninaowaona nimewaingiza mimi kwenye sanaa lakini wao wanajitangaza wameingizwa na mtu fudenge nilishawafuata nikawaambia mbona hunitaji mimi?.

 Si yeye tu na roho yake inamsuta na Mungu na watu baadhi ndo wanajua nani kamfanya yule mtu aonekane kwenye sanaa. Lakini unafiki sitaki, mimi hivyo ndiyo nilivyo siyo mtu wa kujionyesha au kujikuza siyo mtu wa makundi ya kijinga napenda makundi yanayofikiria maisha na yanajua maisha ni nini, sipendi hasa kukaa na watu hawajui kuosha nanilii zao, yule anayejiona Lucy kakosea kuolewa na Mzungu na anifuate aniambie kinagaubaga lakini ukibaki kunisemea pembeni unaniogopa. sikushindwa kuvaa nguo yeyote niliyoipenda mimi au kufanya chochote nilichotaka kama tuliweza kukodi boti kubwa kututembeza visiwa vyote tulivyotaka nisingeshindwa kuvaa chochote ninachotaka, au anayesema ndoa ni kuvaa gauni kuubwa mpaka likuzidi uzito ndiyo ndoa aje aniseme live tukiangaliana?

 Kama mnasema sijui kuvaa kila mtu akijua kuvaa nani atabaki kuwa mshamba? Kila mtu kwenye siku yake special ana-wish kufanya kile alichokitaka sasa mimi nilitaka kusheherekea na watoto yatima na kwenda kisiwani kui-enjoy. Kama Padri angesema umesuka rasta, rasta nimejifurahisha mimi na mume wangu sijafanya kitu kwa kukufurahisha wewe kwani wewe ni nani mpaka nikufurahishe? Padri angetamka siwezi kufungisha ndoa kwa kuwa marafiki au wasanii wenzako hawajaja basi ningelia na kusaga meno lakini loh padri alifungisha ndoa kwa furaha na si tulifurahia ndoa tulipovishana pete na watu wakipiga vigelegele vya furaha basi nimewapiga bao la kisigino loh."

Angalia picha zaidi wakati wa harusi na kitchen party ya Lucy........


Wakila kiapo siku ya ndoa


Boti walikodisha siku ya ndoa
Wakati wa kitchen party
Lucy alibadilisha magauni wakati wa ndoa yake mojawapo likiwemo hili
                                                                              
Like our Facebook page Swahili World Planet for more updates about Tanzanian movie stars' latest gossips, news, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news.

No comments:

Post a Comment