Wasanii wanaounda Club ya Bongo movie Unity wanaendelea kujitoa muhanga kueleza waziwazi matatizo ya Kundi hilo ambalo kwa muda sasa limekuwa likilalamikiwa na wasanii wenyewe na hata watu wengine kuwa halina maana zaidi ya chuki. majungu na kupenda anasa.
Sasa msanii mwingine aliyeamua kufunguka na kujitoa wiki hii ni Flora Mvungi baada ya Esha Buheti. Flora ameandika.....
" Dah..kutokana na mambo yanayoendelea bongo movie club ambayo Kiukweli hayaninufaishi chochote. Zaidi ya kuniongezea chuki kwa watu Bila sababu,Imekuwa ni tatizo kuwa upande wowote Bila malumbano,upendooo,fitna na roho mbaya zinazotengenezwa na sisi wasanii ndani ya club zilinifanya niondoke. Mara ya Kwanza but.!@stevenyerere2 alinishawishi Baada ya kuwa kiongozi nikiona mabadiliko nikarudi ila sasa.! @stevenyerere2 ameng'atuka. Kwasababu ya kutetea wanyonge dah!waliobaki. Ndo wale walionifanya niondoke mwanzo..MAAMUZI magumu sina budi kusema kuwa ni bora nikae mwenyewe nifanye kazi zangu Bila problem Bila kufitinishwa na mtu yeyote..wale ni wasanii wenzangu nawapenda but sera za pale zimenishinda..natangaza. Kujitoa leo Rasmi siwezi migogoro ya Kila siku..! "
Kundi la Bongo movie Unity ni sehemu ya kikundi kidogo tu katika tasnia ya filamu nchini wasanii wa kundi la Bongo movie unity wengi ni wale wenye majina huku wasanii wengi wakiwemo wale wachanga kuweka nguvu na matumaini yao katika Shirikisho la Filamu Tanzania(TAFF) ambalo ndio kubwa na chombo mama cha tasnia ya filamu nchini, mikakati yake ni kupigania maslahi ya wasanii wote na tasnia ya filamu nchini kwa ujumla, TAFF inaundwa na vyama mbalimbali vya wasanii wa filamu nchini lakini kundi la Bongo movie unity inadaiwa sio mwanachama sababu zikidaiwa ni kujiona ni maarufu na kila kitu huku wakiishia. Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania ni Simon Mwakifwamba huku aliyekuwa mwenyekiti wa kundi au club ya Bongo Movie Unity Steve Nyerere akijiuzulu hivi karibuni kwa madai ya kula pesa za kundi hilo kinyume na taratibu
No comments:
Post a Comment