Filamu ya Kitanzania "Dogo Masai" iliyotengenezwa na Timamu African Media chini ya mkurugenzi wake Timoth Conrad inawania tuzo za Silicon Valley African Film Festival katika kipengele cha Best Feature Film.
Inachuana na filamu nyingine toka South Afrca, Nigeria, Malawi, Uganda na Misri. Dogo Masai ni filamu pekee toka Tanzania kuingia katika mashindano hayo na kwa Africa mashariki zikiwa filamu mbili pekee nyingine toka Uganda.
Timoth Conrad amekuwa msanii mbunifu sana nchini kuliko hata wale wakongwe na wenye majina makubwa kwani kazi zake zinajieleza kwa ubora huku akiumizakichwa kila siku. Filamu zake huwa na upekee mkubwa katika ubora pengine kuliko za kampuni nyingine nchini. Licha ya baadhi ya filamu kuuza sana lakini ubora huwa duni sana tofauti na zilizotengenezwa chini ya Timoth Conrad. Hii ni hatua nzuri sana katika tasnia ya filamu nchini kwani mwaka jana pia filamu yake ya Mdundiko ilitamba na kutwaa tuzo hiyo.
Dogo Masai imewakutanishaasanii wenye uwezo mkubwa akiwemo Omary Clayton, Kemmy na Tino Hisani Muya. hiyyo hayo ni trailer ya filamu hiyo ambapo filamu yenyewe bado kuingia sokoni rasm mpaka sasa kwani waandanji wamepanga kwanza filamu hiyo itambe kwenye tuzo kadhaa ndiyo iingie sokoni,
Timoth Conrad anatajia kwenda nchini Marekani muda s mrefu kwenda kuhudhuria tuzo hizo. Ingia hapa ungalie nominees wengine Silicon Valley African Film Festival 2014 Award Nominees
No comments:
Post a Comment