Monday, September 1, 2014

Wema Sepetu Hana Pesa Ya Kunilipa, Nahangaika Ili Tusilale Njaa: Martin Kadinda

Martin Kadinda na Wema Sepetu
Martin Kadinda ambaye ni meneja wa Wema Sepetu ameibuka na kusema kuwa Wema Sepetu aliyekuwa akimwaga pesa vilivyo kwasasa hana pesa ya kumlipa bali yeye Martin anahangaika kwa issue zake binafsi ili wasilale njaa, Kadina alisema kuwa yeye na Wema hawana mkataba wa kulipana bali wapo kishkaji zaidi.
Akizungumza na Visa Martin alisema ......

"Wema hana pesa ya kunilipa mimi, ninachofanya nahangaika kutafuta deals ili mimi na yeye, maisha ni tusilale njaa, maisha ni kutegemeana"

Martin aliongeza kwa kusema "kikubwa ninachofanya ni kutafuta dili za kazi nyingi ili tuwezu kupeana pasu kwa pasu lakini si mshahara, nafanya kazi na bosi wangu Wema kishikaji na kwa kweli nafurahia sana utaratibu huu"

Martin alisema kuwa kama angekuwa na mkataba na Wema kumlipa kila mwezi asingemudu na kusema yupo na Wema kwasababu anajua ni mtu wa aina gani na anafanya akzi zake kwa uhuru bila kubanwa.


Wakati Wema yupo kimapenzi na yule kigogo wa Ikulu aliyejulikana kwa jina la Clement(CK) Wema alidaiwa kumwaga pesa kila kona na wapambe kibao wa kula bata nao hukua akiwa na magari kadhaa lakini kwasasa anadaiwa kushuka kiuchumi na kubaki na gari moja pekee huku wapambe aliokuwa nao wakitimua na waliobaki kulalamika hawali bata kama zamani. Hivi karibuni tena Diamond Platnumz aliye mpenzi wa Wema alisema kuwa Wema ni mtu wa starehe na kuendekeza mashoga wapenda anasa badala ya kutumia fursa na umaarufu mkubwa alionao sasa kufanya kazi zake kwa bidii hususani filamu.


Like our Facebook page Swahili World Planet for more updates about Tanzanian movie stars' latest gossips, news, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news.

No comments:

Post a Comment