Thursday, September 4, 2014

Wema Sepetu Azungumzia Kuhusu Kuajiriwa Na Kajala, Na Meninah Kutoka Na Diamond.


Baada ya mitandao na gazeti moja siku chache zilizopita kutoka na habari kuwa kajala kwasasa ana utajiri mkubwa kuliko Wema Sepetu kiasi cha kuweza kumwajiri Wema anayedaiwa kuwa na pesa za mawazo sasa baada ya kuchezea pesa kipindi cha nyuma. leo Wema kapatikana na kakubali kuongelea isue hizo zote ikiwemo hiyo ya Kajala. 


Kupitia You heard ya  XXL ya Clouds Fm Soudy Brown alianza kwa kutaka kufahamu kama kweli Kajala anaweza kumuajiri yeye [Wema]. Wema Sepetu akamjibu "Inawezekana,kila kitu kinawezekana Soudy"

Kuhusu mshahara ambao anataka kulipwa na Kajala,Wema Sepetu amejibu "Kwa Kajala mi sihitaji mshahara hata bure nitafanya kazi kwa Kajala,shughuli yoyote nitafanya Soudy"
Soudy Brown alipomuuliza kuhusu fununu za Meninah kutoka na Diamond,Wema amejibu "Mimi sijui Soudy bwana na wala sijali"
Msikilize zaidi Wema hapa Mahojiano Ya Wema Sepetu




Like our Facebook page Swahili World Planet for more updates about Tanzanian movie stars' latest gossips, news, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news.

No comments:

Post a Comment