Muigizaji maarufu wa filamu za Kiswahili Tanzania Lucy Komba juzi alifanya kitchen party ya kufa mtu huku asili ya mtanzania ikitawala katika sherehe hiyo. Kila kitu kilikuwa cha asili huku Lucy akiingia ukumbini akiwa ndani ya baiskeli ya magurudumu matatu(guta) iliyozibwa juu kwa nyasi mfano wa kibanda kidogo, na wapambe wake wakiwa wamebeba nyungo. lucy alivaa nguo za bendera ya taifa la Tanzania.
Mastaa wenzake wa filamu walikuwepo kumpa sapoti pamoja na baadhi ya wake wa viongozi mbalimbali. Katikasherehe hiyo hakukuwa na mambo ya keki bali uasili wa Tanzania mpaka katika vinywaji.
Harusi ya Lucy Komba na mchumba wake raia wa Denmark inatarajiwa kufanyika Jumamosi hii.
No comments:
Post a Comment