Thursday, August 21, 2014

Flaviana Matata Achumbiwa Kwa Siri !

Flaviana akiwasalimia wazee kwa kupiga magoti katika tukio hilo
Mwanamitindo maarufu wa kimataifa ambaye pia ni Miss Universe Tanzania 2007 Flaviana Matata anadaiwa kuchumbiwa kwa siri hivi karibuni nyumbani kwao Shinyanga. Picha zimepatikana zikimuonyesha Flaviana akiwa amepiga magoti kuonyesha heshima ya tukio hilo.
Kikizungumza na Globalpublishers chanzo kilisema "Inaonesha hawakutaka watu wajue maana hata hakukuwa na watu wengi siku hiyo, hata hao ndugu wenyewe hawakuwa wengi kiivyo lakini picha zinaonesha Flaviana akichumbiwa,” kilisema chanzo hicho.

Nasikia huyo bwana wake ni Mchaga lakini anaishi Marekani, atakuwa ana fedha zake si mtu wa hivihivi,” kilisema chanzo.

Flavviana alipotafutwa na kuulizwa alikana na kusema sio yeye bali ni dada yake ndiye aliyekuwa akichumbiwa

"Hamna kitu kama hicho,  unayesema alikuwa anachumbiwa si mimi ni dada yangu, mila za kwetu Shinyanga nalazimika mimi kumsindikiza hivyo kama umeona picha hizo uelewe hivyo,” alisema Flaviana.

Hata hivyo, baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo walidai kuwa ni la Flaviana na si dada yake hivyo kuzidi kuzua utata juu ya ukweli halisi, Vile vile inatia shaka kweli kama Flaviana amechumbiwa sasa ikifikiriwa ndiyo kwanza anazidi kukuwa kama mwanamitindo wa kimataifa hivyo kuchukuwa uamuzi wa kuchumbiwa sasa na kuolewa kwa muda huu huwa uamuzi mgumu kwa models wengi wa kimataifa ikifikiriwa bado umri wake sio mkubwa .

Flaviana akiwa kwenye show ya Sherri Hill New York Fashion Week 2012.



No comments:

Post a Comment