Monday, July 14, 2014

Serikali Ikiingilia Kati Wasanii Tutafaidika Sana Na Kazi Zetu: Odama

Muigizaji wa filamu mwenye jina kubwa Odama Jennifer Kyaka amesema kuwa wasanii wanaendelea kunyonywa katika kazi zao kwasababu serikali bado haijaamua kwa dhati kuwasaidia wasanii. Odama aliyasema hayo akizungumza na gazeti moja na kusema kuwa ikiwa serikali itaingilia kati na kuichukulia tasnia ya filamu kama chanzo cha mapato basi wasanii watafaidika vizuri sana na kazi zao kuliko ilivyo sasa hata sheria za serikali hazina nguvu katika kulinda haki za msanii.

Odama pia alisema kuwa filamu yake mpya ya Inside itakuwa moto wa kuotea mbali. Filamu hiyo itatoka tarehe 17 mwezi huu wa July.


No comments:

Post a Comment