Pages

Thursday, July 3, 2014

Johari Akiri Waridi Kumshawishi Kuingia Katika Sanaa Ya Filamu.

Blandina Chagula leo ni jina kubwa kwenye tasnia ya filamu Swahiliwood Tanzania, hata hivyo wengi hawajui kuwa mtu aliyemfanya Johari kushawishika kuingia kwenye sanaa ya uigizaji ni Anna Constantino "Waridi" ambaye alitamba sana na kundi la Mambo Hayo mwishoni mwa miaka ya 1990 na kuvutia watu wengi, Waridi pia amecheza baadhi ya filamu chache kama vile A Point Of No Return akiwa na marehemu Steven Kanumba na Wema Sepetu.

 Kupitia mtandao mmoja wa kijamii Johari ameandika na kuweka picha ya Waridi "dada waridi nampenda sana katika wasanii wa mwanzo walionifanya nipende sanaa na kuamua kuingia huyu alichangia na kupenda sana uhusika wake wa upole na kuteka hisia"

                                                                   Waridi

Like our Facebook page Swahili World Planet for more updates about Tanzanian movie stars' latest gossips, news, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news.

No comments:

Post a Comment