Pages

Thursday, July 3, 2014

Jackline Wolper Aopoa Bwana Mpya ! Ni Model Wa Kibongo, Watumiana Ujumbe Wa Kimahaba.

Casillah na Jackline Wolper
Baada ya kumwagana na G-model, star wa filamu nchini Jackline Wolper  anadaiwa kutoka kimapenzi na jamaa mwingine anayeitwa Casillah ambaye ni model wa Tanzania na mwaka jana alishiriki shindano la Mr.Tanzania ingawa aliangukia pua. Jana Swahiliworldplanet ilitonywa na star mmoja wa filamu kwa kusema "unamjua bwana mpya wa Wolper?....njoo nikuonyeshe, jamaniii Wolper!"

Baada ya kuonyeshwa picha za jamaa huyo ambaye sio mgeni machoni pa SWP haraka ilimsaka kwenye Instagram na kukuta ameandika ujumbe wa kimapenzi kuhusu Wolper na kuweka picha yake. Ujumbe huo ulisomeka "If I could take all girls in this world and put them in one room, none of them can compare with You, You got everything, you got everything I wanted and you are still the one to me my princess"

Nae mpashaji huyo alisema kuwa Wolper pia aliweka picha ya jamaa huyo na kuweka caption Instagram lakini baada ya dakika chache aliondoa picha na ujumbe huo bila kukwapuliwa na mtu.

Hata hivyo Wolper hakupatikana kutolea ufafanuzi ila tutakuletea atakachosema
                                                                Casillah
Like our Facebook page Swahili World Planet for more updates about Tanzanian movie stars' latest gossips, news, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news.

No comments:

Post a Comment