mwenyekiti wa Bongo Movie Unity Steve Mengere "Nyerere" |
- Kwa mtu yoyote anayefuatilia skendo zinatokea katika sekta ya FILAMU hasa kwa hawa wanaojiita mastaa atakubaliana nami kuwa sekta hiyo inahitaji mtu makini na sahihi kuiongoza ili kuiletea mabadiliko ya kweli.
-Ndiyo maana wanafila
mu wenyewe wakaonelea ni vyema wakaanzisha harakati za kujikomboa zilizozaa SHIRIKISHO LA FILAMU ( TAFF ) na vyama vyake mbali mbali vinavyoyokana na taaluma zilizoko ktk FILAMU.
-Jambo la kushangaza kuna kitu kingine kimejiweka pembeni na hizo harakati kinajiita BONGO MOVIE.
-BONGO MOVIE imekuwa ikifanya kila linalowezekana kuhakikisha SHIRIKISHO FILAMU halifikii malengo yake, iwe kwa mbinu za siri ama dhahiri ikiwemo ile ya kujifanya hawana matatizo na SHIRIKISHO LA FILAMU wala VYAMA VYAKE,bila kujuwa kuwa na wenyewe ndani si wamoja.
-BONGO MOVIE ilikutana na wakati mgumu sana ilipokuwa ikiongozwa na JACOB STEPHEN akiwa mwenyekiti HARTMAN MBILINYI akiwa makamu wake na ISSA MUSSA CLOUD yeye akiwa kama katibu mkuu wa taasisi hiyo,lakini pia hali hiyo iliendelea hata pale ilipokuwa ikiongozwa na VICENT KIGOSI ,SALUM MCHOMA (CHIKI) SIMON MWAPAGATA ( RADO ).
-Tatizo kubwa likiwa ni kashfa, dharau,kebehi na matusi kutoka kwa wasanii na hasa wa kike ambao walikataa kabisa kutii amri za uongozi bila waliokuwa wakitoa amri hizo kujuwa kuwa aliyekuwa akiwatuma kuonyesha jeuri hiyo alikuwa ni STEVEN NYERERE kwa kuwa alikuwa na ushawishi mkubwa kwao kutokana na kuwa kuwadia kwa watu mashuri na wenye fedha.
-Jambo la ajabu taasisi hiyo kwa sasa inahaha kuhamisha watu kutoka SHILIKISHO LA FILAMU na tayari imekwisha mnasa aliyekuwa mwenyekiti wa chama cha waigizaji taifa MIKE SANGU na Mkewe NDUMBAGWE MISAYO ( THEA ) na tayari SANGU amekwisha waahidi kuifanya kazi hiyo na walengwa wa awali ni LUMOLE MATOVOLWA ( BIG ) na DAVID ELIYA MJATA huku LUMOLE akiahidiwa kuwekwa nafasi ya JACOB STEVEN ( J B ) katika kazi za uigizaji yaani nafasi ya baba.
-Tatizo langu liko kwenye malengo ya BONGO MOVIE ambayo utekelezaji wa STEVE NYERERE ambaye ndio kiongozi wake kwa sasa umekuwa wazi mno kulingana na nilicho kifahamu toka awali kuwa inahitaji watu wa kuwatumia kama TOILET PAPER na ikishamaliza matumizi inawaacha ,Haya yanadhihiri kwenye kauli iliyotumika kumnasa mmoja kati ya wana TAFF
-Aliyeambiwa kuwa hata MIKE SANGU wanamuhitaji tu ili wapate kundi kubwa la watu litakalotumika kumshawishi mmoja kati ya wanaotajwa kuwania uraisi wa jamuhuri ya muungano wa tanzania litakalowasaidia kupata pesa kutoka kwa mgobea huyo na si vinginevyo.
-Haya yalijiri kwa marehemu STEVEN KANUMBA ambaye baadae aligeuka kuwa adui na sasa kwa JACOB STEVEN kama ambavyo anatarajiwa MIKE SANGU anayeitwa msaliti.
-Ni STEVE NYERERE huyu huyu ndiye aliyesikika akisema kuwa ndani ya BONGO MOVIE wapo baadhi yao ni mashoga tena bila kuwataja mashoga wenyewe ili apate kuwadharilisha anaowataka yeye jambo ambalo linatia kinyaa,Lakini kubwa kuliko yote ni pale aliposema kuwa anashangazwa na utitiri wa maproduza ndani ya BONGO MOVIE Eti hata JIMMY MAFUFU naye ni PRODUZA, kiasi cha kutaka kuwapunguza,Sifahamu hapo yeye akiwa kama nani na hapo ndipo niliposhawishika kuigusa dhana ya KARLPETERS na CHIFU MANGUNGO.
-Nawaonya ndugu zangu wanaokimbilia huko ni vyema kabla ya yote ukajifunza kupitia wanaokujua kuhusu hali ya maisha ilivyo huko si mahala salama kwa mtu mwenye malengo na anayejiheshimu kama huamini nenda kamuulize PACHO MWAMBA aliyo yapata kutoka kwa marehemu STEVEN KANUMBA .
source: Mkombozi Wa Wanafilamu.
Like our Facebook page Swahili World Planet for more updates about Tanzanian movie stars' latest gossips, news, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news
No comments:
Post a Comment