Pages

Monday, June 30, 2014

Ndoa Ya 3 Ya Dida Na Ezden Yavunjika ! Dida Apokea Kichapo Na Kudai Talaka.

Dida na Ezden
Ndoa ya Tatu ya mtangazaji maarufu nchini Khadija Shaibu "Dida" ambaye pia ni muigizaji wa filamu imevunjika !. Kwa mujibu wa Globalpublishers Dida na mumewe Ezden ambaye ni mtangazaji wa TVI wapo kwenye ugomvi na juzi Dida alipigwa na mumewe huyo kisha mume kuondoka nyumbani na begi lake la nguo. Dida amekiri kupigwa na kusema anataka talaka yake
"Mimi na mume wangu huwa hatuna mipaka katika simu zetu, kila mtu yuko huru kuchezea simu ya mwenziye. Siku ya tukio jamaa (Ezden) kabla hajaenda kuoga alitengeneza namba za siri (pasword) sasa nilivyotaka kucheza gemu nikamfuata bafuni na kumuuliza mbona simu imefungwa, nikamuomba anifungulie, huwezi amini akaanza kunitukana, nikajiuliza ni simu tu au kuna mengine" Alisema Dida ambaye alitamba na tamthilia kadhaa za Kaole

Aliendelea kwa kusema "Nilishangaa sana, nikajiuliza kosa langu ni nini? Alinipiga hadi akanipasua sehemu ya kichwa, sikuamini kama Ezden anaweza kunifanya vile au kama alinichoka angeniambia wakati yeye ndiye mkosaji"

Dida amesema kuwa anachotaka sasa ni talaka yake na alishindwa kumuomba mumewe huyo msamaha siku ile ile. Ukiachilia mbali ndoa hii ya Dida iliyo kitanzini, huko nyuma alifunga ndoa na Mohamed Mchopanga na Gervas Mbwiga "G" na kisha wote kumuacha kwa talaka.
Dida na Ezden
Like our Facebook page Swahili World Planet for more updates about Tanzanian movie stars' latest gossips, news, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news

No comments:

Post a Comment