Pages

Monday, June 30, 2014

Diamond Hujanionea Justine Bieber Huko BET Awards 2014: Lulu

Lulu
Inaonekana Star wa filamu mwenye makeke mengi nchini Elizabeth Michael "Lulu" ana matumaini ya kukutana na Justine Bieber na kumueleza lililo moyoni mwake kuwa anampenda !. Mwaka 2011 wakati akifanya mahojiano na Zamaradi Mketema alisema kuwa alikuwa na nia ya kwenda Marekani kumuona Justine Bieber kwa kuwa anampenda sana na yupo tayari kwa lolote lile. Mwishoni mwa mwaka jana tena akatoa dukuduku lake tena kuhusu Bieber kupitia twitter ingawa tweet hizo aliziandika kwa Kiswahili.

Sasa basi, leo kupitia Instagram Lulu ameamua kumuuliza Diamond Platnumz kama hajamuona Justine Bieber hata kwa mbali tu kwenye tuzo za BET Awards 2014 ambazo Diamond alikuwa nominated na kuhudhuria. Lulu alipost picha ya Diamond akiwa na star wa Marekani Nelly halafu akampongeza Diamond na kuandika "Hongeza sana Brother....dah sio mwenzetu tena we Diamond Platnumz yaani I saw kwa macho na naniliuu......kushiriki kwako ni ushindi tosha.....sema nini Justine Bieber hujanionea hata kwa mbali brother"

Inaonekana Lulu akipata nafasi ya kuhudhuria event ya Hollywood atahakikisha anamsaka Justine Bieber huko huko ...lol
                                                              Diamond na Nelly
Justine Bieber
Like our Facebook page Swahili World Planet for more updates about Tanzanian movie stars' latest gossips, news, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news

No comments:

Post a Comment