Wema Sepetu |
Kwa mujibu wa chanzo kimoja kilicho karibu na Wema kimesema kuwa filamu hiyo yupo pia Aunty Ezekiel na Hemedy. "kuna uwezekano Wema akalipwa mil.90 kuuza movie yake mpya alocheza na Aunty na Hemedy na ......(akimtaja msambazaji) lakini hawajamalizana bado unajua wasambazaji wengine wamemfata madam pia but yeye hayupo tayari kuuza kwa bei ndogo kama wengine, si unajua sokoni anauza fresh" kilisema chanzo hicho kwa masharti ya kutotajwa jina
Hata hivyo Wema hakupatikana kuzungumzia suala hilo ingawa takribani mwezi mmoja uliopita mmoja wa maproducer wa filamu nchini alisema pia kuwa amesikia kuwa Wema atalipwa pesa nzuri kwa filamu yake mpya anayo-shoot akiwa na Aunty Ezekiel na Hemedy ingawa habari hiyo haikuandikwa. SWP ilipojaribu kumuuliza mmoja wa wafanyakazi wa kampuni hiyo alisema hajui hilo na pia yeye siyo mzungumzaji wa kampuni kwa hiyo hana lolote la kusema kama ni kweli au sio kweli.
Wema |
No comments:
Post a Comment