Pages

Thursday, June 26, 2014

Irene Uwoya Kumuweka Kitako Ray Kwanini Amemwaga Johari Na Kutoka Na Chuchu Hans.

Irene Uwoya
Actress Irene Uwoya amekuwa mshauri wa mambo ya mahusiano ya kimapenzi !......well, habari mpya ni kuwa baada ya Ray kudaiwa kumwaga Johari kimapenzi ambaye pia kwa pamoja wanaimiliki RJ Films Company na kuangukia kwenye penzi la actress mwingine Chuchu Hans, Uwoya anadaiwa kutaka kumuweka kitako Ray kumuuliza ni kwanini amemwaga shosti yake Johari na kuamua kutoka na Chuchu ambaye wanadaiwa kufunga ndoa ya siri na Ray hivi karibuni na kuanza kuishi pamoja. Chanzo kimoja kilicho karibu na Johari na Uwoya ambao ni mashosti wa kutupwa kwasasa kikizungumza na Swahiliworldplanet kilisema
"Unajua Johari na Uwoya ni mashosti wakubwa, wamefanya kazi nyingi pamoja, Uwoya hajapendezwa na kitendo cha Ray kumwaga shoga'ke na kisha kutoka na Chuchu, Johari hana amani kwa muda mrefu tangu wapigane na Chuchu ofisi za RJ anaamini Ray ni wake siyo wa Chuchu, Uwoya anataka kumkalisha kitako Ray ili Johari awe na furaha kama zamani" kilisema chanzo hicho na kuomba kisitajwe jina lake

Hata hivyo SWP ilijaribu kumtafuta Uwoya ili kumuuliza lakini namba yake haikuwa hewani huku Johari na na Chuchu wakishindwa kufikiwa, kwa upande wa Ray mara nyingi anapotumiwa ujumbe ili kutolea ufafanuzi habari zinazomhusu huwa hajibu.
                                                                         Johari
                                                              Ray na Chuchu
Like our Facebook page Swahili World Planet for more updates about Tanzanian movie stars' latest gossips, news, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news

No comments:

Post a Comment