Pages

Thursday, June 26, 2014

Diana Kimaro Arudi Shule Kuendelea Na Kidato Cha Tano.

Diana Kimaro
Muigizaji wa filamu nchini aliyejipatia umaarufu licha ya kuwa na umri mdogo Diana Kimaro amesema kuwa amerudi shule kuendelea na kidato cha tano ili kwakuwa elimu ni muhimu na hawezi kufanya maisha ya anasa wakati huu ndiyo muda wake wa kupata elimu ya kutosha.
Akizungumza na gazeti moja Diana anayetamba sokoni na filamu ya Kigodoro na Foolish Age akiwa na Elizabeth Michael "Lulu" amesema kuwa anasoma ili elimu imsaidie kufikia malengo yake kisanaa kufanya filamu za kimataifa tofauti na ilivyo sasa. Diana Pia amewashauri waigizaji wenzake kuongeza elimu zao ili kuifikisha sanaa ya filamu Tanzania mbali. Hata hivyo Diana amesema kuwa anasoma huku anaendelea kufanya filamu kama alivyokuwa akifanya mwanzo kudhibiti muda wake wa elimu na filamu.
                                                               Diana Kimaro
Like our Facebook page Swahili World Planet for more updates about Tanzanian movie stars' latest gossips, news, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news

No comments:

Post a Comment