Monday, June 16, 2014

Bongo Movie Unity Acheni Ustaa Bali Unganeni Na TAFF Katika Harakati Za Kweli Kuikuza Kitaalam Tasnia Ya Filamu Tanzania.

baadhi ya wasanii wa kundi la Bongo movie unity
Rais Kikwete amesema kuwa mwezi ujao yaani July atawaleta Trey Songz na Unsher Raymond toka marekani kuja kutumbuiza nchini na pia kuzungumza na wasanii wa filamu na muziki. Kwa mtazamo wangu ni kuwa kama kweli Rais angekuwa na wasaidizi na washauri wazuri asingefikiria kuwaleta hao wasanii sasa kwasababu wameshakuja wengi na tumewaona bila kuwa na impact ya kueleweka kwenye industry bali kufuja pesa tu za walala hoi. Nafikiri kama ana washauri wazuri kuhusu sanaa ya Tanzania basi wangejikita katika kujenga msingi mzuri wa wasanii wa nyumbani, msingi mzuri wa vyuo vya elimu ya filamu na mzuiki, kutengeneza sera na sheria nzuri za filamu na muziki, kupunguza na kuzuia uharamia kabisa, media za nchini kutoa kipaumbele kwa wasanii wa Tanzania na sio wa nje kama ilivyo sasa, mfano Nigeria ni vigumu wasanii wa marekani kupewa kipaumbele hata kama kazi zao ni nzuri kitu ambacho kimeifanya sanaa ya filamu na muziki Nigeria kukua kwa kasi ili wasanii wafaidike na kazi zao.

mwenyekiti wa kundi la Bongo movie unity Steve Nyerere
Usher na Trey Songz ni wanamuziki watazungumzaje mambo critical kuhusu filamu na wasanii wa filamu Tanzania?. Brazil ililetwa nchini na mabilioni kutumika je Tanzania ilifua dafu michuano ya kombe la mataifa ya Afrika na sasa kombe la dunia? jibu ni kuwa waliletwa na kutumia pesa bila sisi kujijengea msingi mzuri hata huyu Usher na Trey Songz watakuja watazungumza maneno mawili matatu kwa siku moja na kula mabilioni ya pesa kisha kusepa kwao na sisi tukibaki kupiga picha nao. Katika hili sijui kama TAFF imetaarifiwa, kundi la Bongo Movies Unity nalo halijitambui kabisa linafikiria kusaidiana kwenye misiba na harusi pekee ndiyo kukua kwa tasnia na njia ya kuishawishi serikali iwe active kwenye tasnia ya filamu nchini. kwa mtazamo wangu kundi hili lina wasanii maarufu lakini wenye upeo mdogo kuhusu sanaa ya filamu kuliko ilivyo TAFF ambayo ina wasomi, Bongo Movie Unity pia lina wasanii wanaopenda kujionyesha mbele za media na watu, kundi ambalo hata kisheria halitambuliki.
Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania(TAFF) Simon Mwakifwamba
Wasanii wa kundi la Bongo movie Unity wanatakiwa kuungana na TAFF katika harakati za kukuza na kushawishi serikali iwe active kuisadia hii tasnia. wengine wanailamu TAFF eti matokeo mazuri mpaka sasa hayajaonekana bila kujua kuwa kufuatilia sera, kurasimisha sector na kuunda sheria sio kazi ya wiki moja kama ilivyo vikao vya harusi za Bongo movies . Bongo movie unity wanatakiwa wajue kuwa Hata Hollywood na Bollywood kuna mastaa wakubwa kuliko wao lakini nyuma ya mastaa hao wakubwa wa Hollywood kuna wasomi walio nyuma yao ambao hata hawajulikani kwa watu ila mchango wao ni mkubwa sasa kwa kufanya mambo na mikakati ya kisomi kuhusu tasniaya filamu, Serikali haiwezi kushawika au kuzuzuliwa na umaarufu wa Wema Sepetu, JB, Ray , Lulu au Wolper katika kujenga sera, mikakati na sheria za filamu bali kuna mambo na taratibu za kufuata ambazo TAFF ndiyo inafanya sasa na huchukua muda na kuhitaji subira.
baadhi ya wasanii wa kundi la Bongo movie
Ukiangalia na kusoma matamshi ya kiongozi wa Bongo Unity Steve Nyerere katika media mara nyingi huwa unapatwa na wasiwasi kuwa kama huyu ndiye kiongozi mambo yatakuwaje huko mbeleni. Steve amekuwa akituhumiwa na wasanii wenzake hasa wa kike kuwakuwadia kwa wafanyabiashara wakubwa na vigogo wa serikali na yeye mwenyewe kushindwa kutoa utetezi wenye nguvu za hoja kuhusu hilo, pia zaidi ya mara moja Steve Nyerere ambaye ni mwenyekiti wa kundi la Bongo movie unity amekaririwa akisema kuwa yeye hataacha kuwapiga mizinga(kuwaomba pesa) viongozi na wafanya biashara wakubwa anapokutana nao kwakuwa wanazo pesa, pesa hizo sio kwa ajli ya kujenga tasnia but issue binafsi tena za kistarehe zaidi sio za kimikakati ya kuijenga tasnia kitu ambacho hata baadhi ya wafanya biashara na vigogo wameshakaririwa magazetini wakilalamikia suala hilo na kusema wasanii wa bongo movie ni omba omba.
katika hilo Jackline Wolper na baadhi ya wasanii wengine wa kike walisema kuwa wenye tabia hiyo ni baadhi ya wasanii wa kiume ila wanasingiziwa wao wasichana na siku chache baadaye Steve alipoulizawa na gazeti moja alikiri kufanya hivyo na kusema hataacha kuwaomba waheshimiwa anapokutana nao kwani wanzo, hii ni kauli ambayo haikupaswa kutamkwa na kiongozi kwani si tu kuwa anawashusha wasanii anaowaongoza bali wanadharaulika pia wakati sio wote wenye tabia hizo. Ukipima upeo wa Steve Nyerere na na Mwakifwamba Simon ambaye ni Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania utaona tofauti kubwa, mwakifwamba anaonekana ni msomi na mwenye upeo hata katika maandishi na matamko yake kwenye media. Bongo movie unity acheni kuongozwa na ustaa hauna nguvu katika maendeleo ya tasnia ya filamu Tanzania kama hamtajishusha na kuwa chini ya TAFF ambacho ndiyo chombo mama cha filamu Tanzania.
Bishop Hiluka, mmoja wa viongozi wa TAFF na msomi mwenye upeo wa hali ya juu kuhusu tasnia ya filamu
Kwa kumalizia ni kuwa ukiachilia mbali kujenga msingi mzuri wa elimu ya sanaa ya filamu na muziki, sera na sheria, Rais kikwete angefikiria kuwaleta mabingwa wa sera za filamu na muziki toka Marekani, wachumi na wasanii wawili watatu kwa pamoja waungane na viongozi wa TAFF na wale wa muziki Tanzania na wasanii wenyewe katika mipango ya muda mrefu katika kuikuza sanaa ya Tanzania, na katika hili kama wakija hao watu toka Marekani wakiachiwa kundi la Bongo movie unity pekee lazima watachemsha tu kama TAFF haitahusishwa kwa asilimia kubwa kwani ina wasomi na watu wenye weledi kuhusu Tasnia.
Hayo ni maoni katika kujenga sanaa yetu sio chuki wala wivu na nimejaribu kuweka mada mbili tofauti katika sehemu moja.

Like our Facebook page Swahili World Planet for more updates about Tanzanian movie stars' latest gossips, news, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news

No comments:

Post a Comment