Thursday, May 1, 2014

Yusuph Mlela Adaiwa Kuwa Teja. Mwenyewe Afunguka.

Star wa filamu Swahiliwood Yusuph Mlela anadaiwa kuwa teja(kutumia madawa ya kulevya) kiasi cha kushindwa kujichanganya na wasanii wenzake katika matukio mbalimbali ya kijamii. Chanzo kimoja kikizungumza na GPL kilisema kuwa Mlela kwasasa anaonyesha waziwazi kuwa ni mtumiaji wa madawa ya kulevya.
Hata hivyo Mlela mwenyewe alipotafutwa na Globalpublishers na kusomewa mashtaka yake alisema "Katika maisha yangu sijawahi kutumia madawa ya kulevya na huwa nayapinga sana. Wanaosema navuta ni waongo, mimi sasa hivi naitwa baba, hivyo majukumu yameongezeka ndiyo maana sijichanganyi kivile"

No comments:

Post a Comment