"Nashkuru Mungu na wote mlioniunga mkono mpaka hapa nilipo kisanaa, Sasa ni wakati wangu wakufanya kile kilichonitoa Congo kuja Tanzania, muda wowote kuanzia sasa naweza kuanza kufanya filamu zangu Afrika nzima, kuanzia Congo, Rwanda, Burundi, Uganda, Kenya na Tanzania, Sijaja kuuza Sura kwenye tasnia ya filamu Tanzania, nashukuru maana Filamu nilizocheza zinanipa Umaarufu mkubwa ndo sababu ya kukamilisha ndoto zangu, Kwa ushauri na mengineo, Wasiliana na mimi Modest Bafite bila tatizo, ikiwa hujawahi kuona filamu zangu niulize nitakwambia title ya Filamu ambazo nimecheza, mnakaribishwa kwa maoni"
Kwa upande mwingine filamu mpya ya Modest inayoitwa SIO SAWA itaingia sokoni muda wowote kuanzia sasa ambapo amecheza na mastaa wenzake kama vile King Majuto, Babylove Kalalaa na Salehe Lufedha ambaye ndiye producer wa filamu hiyo kali.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
No comments:
Post a Comment