Thursday, May 1, 2014

Film Review: Hukumu Ya Ndoa Yangu - JB Ashindwa Kuonekana Kama Mwanafunzi Wa College, Bi.Mwenda Angara.

FILM: Hukumu Ya Ndoa Yangu.
CAST: Jacob Stephen, Shamsa Ford, Fatma Makongoro, Wellu Sengo, Mayasa Mrisho, Annasiri Msangi
DIRECTOR: Adam Kuambiana
RATING: 2.5/5

Hukumu Ya Ndoa Yangu ni filamu mpya kutoka Jerusalem Films inayomilikiwa na Jacob Stephen"JB". Katika hii filamu JB ni mwanafunzi wa chuo akisomea mambo ya uhasibu pamoja na rafiki yake(Chiki Mchoma). JB analipiwa ada na mama yake ambaye ni Fatma Makongoro"Bi.Mwenda" ambaye pia anaishi na mabinti zake wawili akiwemo Mayasa Mrisho huku familia yao ikiwa masikini, JB anasisitiziwa na mama yake kuhusu kusoma kwa bidii. Mara nyingi wanapokuwa chuoni JB na Chiki huenda kula kwa mama ntilie(Annasiri Msangi) ambaye anasaidiwa na Shamsa Ford ambaye ndiye muigizaji mkuu wa kike katika filamu hii. Shamsa alikuwa binti wa mtaani baada ya kuzaliwa na mama yake ambaye hakuwa na akili sawa sawa ambapo alibakwa na matokeo yake kuzaliwa Shamsa na kuwa mtoto wa mtaani ambaye baadaye anachukuliwa na mama ntilie(Annasiri Msangi) na kukaa nae kama mama yake. JB anampenda Shamsa lakini Chiki anasema sio hadhi yake yeye akiwa kama msomi, Annasiri Msangi anamuonya binti yake huyo wa hiari kuwa makini na wanachuo kwani wengine watamchezea na kumtelekeza.

 Baadaye Shamsa na JB wanakuwa wapenzi na Shamsa kupata mimba na JB kukataa ujauzito huo. Shamsa anaenda kumueleza mama yake ambaye anakuja juu kuwa itakuwa aibu akiwa kama mmoja wa viongozi wa kanisa. Wanafunga safari mpaka kwa mama yake JB yaani Bi.Mwenda na kumueleza. Yeye pamoja na mabinti zake wanawatolea maneno ya shombo Shamsa na mama yake pamoja na JB mwenyewe. Hata hivyo Shamsa na JB wanaishi pamoja na kumlea mtoto wao kwa shida huku wakiuza genge ili waishi. Baadaye JB anapata kazi nzuri na kuhamia  kwenye nyumba nzuri, Shamsa anamwomba mumewe awachukue mawifi za mama yake mkwe waishi wote ambapo wanaendeleza visa huku mama mkwe akitaka Wellu Sengo ambaye ni sekretari wa JB awe mkwewe na JB kupinga. Dada yake JB mmoja wapo anapanga njama na Q-Chief ili ajifanye yeye na Shamsa ni wapenzi ili JB awafumanie na kumwacha Shamsa, JB alipowafuma anazimia na filamu kuisha.

What is good: Mwandishi alijaribu kuonyesha  visa vya mawifi na mama mkwe katika familia nyingi hata kama wahusika wenyewe wanapenda lakini wao wanataka kuwatenganisha. Wasanii walicheza vizuri sana hasa Bi.Mwenda alikaa vizuri sana kwenye nafasi yake kama mama mkwe mwenye roho mbaya na anayeamini imani za kishirikina. Shamsa Ford pia alicheza vizuri katika nafasi yake kuazia kuwa mama ntilie, Annasiri, Mayasa Mrisho na dada yake Mayasa walicheza vizuri pia.

What is bad: Mwandishi wa story na script hakufanya kazi nzuri huku filamu ikiisha bila kueleweka vizuri kuhusu mwisho wa Shamsa ambaye hakuwa na hatia na mwisho wa Bi.mwenda na mabinti zake, filamu inaisha ghafla bila kutarajia. Director wa filamu hii pia hakufanya kazi sawasawa . mfano wakati JB yupo darasani alipotoka kulikuwa na mtu mbele yake aliyeonekana kuikimbia kamera ili kuwapisha waigize. Kingine ni JB kushindwa kuonekana kama mwanafunzi wa college, umbo na muonekano wake havikushawishi kabisa kuwa ni mwanafunzi hasa wakati yupo darasani akijisomea huku wanafunzi wenzake wakionekana kama mwalimu wao ni huyo JB au ni mfanyakazi wa chuo, hapa kwa wenzetu kama Hollywood au Bollywood kungekuwa na maandalizi ya mhusika mfano kupungua uzito ili kuendana na uhusika wake, kwa ufupi character ya uwanafunzi katia filamu hii haikumkaa JB ingawa baadaye alipoigiza kama baba wa familia na mhasibu alikaa vizuri. Hata Chiki pia hakuwa anashawishi kama mwanafunzi wa chuo.

Last Word Of The Film: Katika hii filamu kivutio kikubwa ni B.Mwenda ambaye aliuvaa uhusika wake vizuri sana, nunua hii filamu umuangalie bila kuwasahau Shamsa Ford, Annasiri Msangi na Mayasa Mrisho ili ujionee visa vya mama mkwe na mawifi.

xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Filamu kali ya SIO SAWA inaingia sokoni Ijumaa hii April 2014 hakikisha unanunua nakala yako halisi.
Follow us on twitter Swahili World Planet  and Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, beauty, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news, life styles news and more

No comments:

Post a Comment