Wednesday, April 30, 2014

Photos: Nisha Achaguliwa Kuwa Balozi Wa Steps Solar Na Kuungana Na JB, King Majuto Na Irene Uwoya.

King Majuto, Nisha na JB
Star mkubwa wa filamu nchi Salma Jabu "Nisha" amekuwa balozi wa kampuni ya Steps Solar ambayo hujishughulisha na uuzaji wa umeme wa jua wa bei nafuu na pia vifaa vinavyotumia umeme huo. Hii ina maana kuwa ukinunua vifaa vya umeme vya steps na huduma zao nyingine za umeme wa jua basi una uwezo wa kutumia kifaa chenye umeme seheme yoyote ile hata porini bila kuhitaji umeme wa Tanesco. Nisha ameungana na mastaa wenzake King Majuto, Jacob Stephen(JB) na Irene Uwoya ambao tayari walikuwa mabalozi wa kampuni hiyo. Uzinduzi na kutambulishwa kwa wasanii hao kama mabalozi ulifanyika leo ingawa Irene Uwoya hakuwepo loe. Swahiliworldplanet ilifanikiwa kumuuliza maswali kadhaa Nisha kuhusiana na ubalozi wake huo kama ifuatavyo


SWP: Kwa hiyo wewe King Majuto na Jacob Stephen "JB" nyote ni mabalozi au ?

NISHA: Mwanzo walikuwa JB, Uwoya na Majuto sasa hivi nimeongezeka mimi kama balozi wa Steps Solar umeme bora na rahisi kutumia usio na gharama kubwa na hauna mgao.
baadhi ya vifaa na bidhaa za Steps Solar


SWP: .Steps Solar inajihusisha na nini na kazi zenu kama mabalozi zitakuwa zipi?

NISHA: Hizo ni baadhi ya bidhaa zinazotengenezwa na kampuni ya steps solar kama unavyoziona hapo kuna mafriji,maji yanayotumia nishati nuru ukame sasa kushinehi,kama mabalozi kazi yetu Kubwa ni kuwakomboa wananchi wa hali ya chini hususan na hizi adha za umeme na maji,kama tujuavyo ndio vitu vya msingi katika jamii,binafsi napenda sana kufanya kazi za kijamii naamini hapa ndipo nakamilisha msemo wa kioo cha jamii
Baadhi ya bidhaa za Steps

Kwa kiasi fulani ndio hiyo moja na pili pia tutatembelea mikoa na vijiji mbalimbali kusaidia wananchi haswa wale wenye shida hasa, ila pia hata wa mjini au mtu yyte anatakiwa atumie Steps Solar hasa hasa kulinda uchumi na matumizi yasiyo ya lazima ili tuzidi kuijenga nchi yetu Kwa kutumia chanzo asilia cha nishati nuru
SWP: Mkataba wenu ni wa muda gani na vipi kuhusu malipo ya mkataba wenu unayaonaje?

NISHA: Malipo ni mazuri sanaaaaaa ha ha ha na mkataba kwa sasa siwezi zungumzia ni wa muda gani ila kwangu mimi nahisi hadi watanzania watakapomaliza hii adha ya umeme na maji na vifaa vya bei rahisi vinavyouzwa na steps solar ambayo utazipata maduka yote yanayouza Bongo movies au ulizia maduka yaliyo karibu yako.
Mbunge wa Kigamboni pia alikuwepo

SWP: Una chochote ungependa kuongeza kuzungumzia?

NISHA: Sina, cha zaidi, ila nina suprise kubwa tarehe1 watege macho na masikio mashabiki zangu wapenzi

Angalia picha zaidi....................







No comments:

Post a Comment