Thursday, March 13, 2014

Wema Sepetu Na Aunty Ezekiel Washushiwa Kichapo Cha Haja Na Adam Kuambiana Baada Ya Kumtolea Maneno Ya Shombo.


Mastaa wakubwa wa filamu Swahiliwood Wema Sepetu na Aunty Ezekiel wamepokea kichapo cha haja kutoka kwa muigizaji mwenzao Adam Kuambiana ambaye pia ni director wa filamu nchini. Kwa mujibu wa Globalpublishers Tukio hilo lilitokea maeneo ya Mikocheni jijini Dar es salaam ambapo wasanii hao walikuwa wakishuti filamu ambayo inaongozwa na Adam Kuambiana. Wema na Aunty walipokea kichapo baada ya kumtolea maneno ya shombo Adam kwa kumwambia kuwa kucha zake za miguuni ni ndefu sana anatakiwa azikate tena kwa kutumia mkasi wa kukatia michongoma na sio kwa kutumia kiwembe.


 Wema ndiye aliyeanza kummwagia Kuambiana maneno ya shombo akimwambia kuwa ahakikishe siku hiyo haipiti bila kukata kucha za miguuni kwani ni ndefu na zinatisha.
"Mwanzoni ilikuwa kama utani tu,Wema alimwambia Kuambiana akate kucha tena itabidi atumie mkasi wa kukatia michongoma maana kwa wembe hazikatiki, Pia Wema alimwambia yeye hawezi kumwacha mpenzi wake na kucha ndefu kama hizo za Kuambiana" kilisema chanzo kikizungumza na GPL

Aunty Ezekiel na Wema Sepetu

Baada ya Wema kutoa maneno hayo kwa Kuambiana Aunty nae alidaiwa kudakia na kumpaka zaidi Kuambiana kuwa ana kucha ndefu na zinahitaji kukatwa kitu kilichopelekea Kuambiana kushindwa kujizuia na kunyanyuka kwenda kutoa kichapo cha haja. "Baada ya kuona imekuwa ‘too much’, Kuambiana alipandwa na hasira, akanyanyuka kwenye kochi na kumfuata Wema kwa lengo la kumpa kipigo" kilisema chanzohicho.

Kuambiana alipomfikia Wema na kuanza kumchapa vibao vya maana Martin Kadinda ambaye ni meneja wa Wema aliingilia kati kujaribu kumuokoa Wema. Baada ya kumaliza kumpa kipigo Wema alimgeukia Aunty na kuanza kumlamba makofi ya kutosha huku wasanii wengine waliokuwa eneo hilo wakidaiwa kukimbia wakishindwa kuwatetea wema na Aunty kuogopa nan wao kupewa kichapo na director huyo anayejulikana kuwa na mkono mwepesi kwani kipindi cha nyuma aliwahi kumshushia kipigo Rose Ndauka wakati walipokuwa Zanzibar kushuti filamu.

Adam Kuambiana

Kuambiana alipotafutwa na na GPL na kuulizwa kuhusu issue ya kutoa kichapo cha mbwa mwizi kwa wasanii hao alikiri kwa kusema kuwa Wema na Aunty ni kama wadogo zake lakini walipomshushia heshima ndipo akawashikisha adabu."Akina Wema ni wadogo zangu, wanahitaji kuniheshimu na mimi ndiye mwongozaji wa filamu yao, kwa nini wanikosee heshima? Hata kama wamekasirika lakini nimewashikisha adabu"


Wema na Aunty ambao ni marafiki wakubwa kwa muda mrefu sasa walipoulizwa kuhusiana na kichapo walichopewa walisema walishamzoea Kuambiana lakini kwa alilolifanya la kuwapiga makofi  aliwakwaza kwa sababu hata kama ni mwongozaji wa filamu yao lakini alikuwa pale kwa ajili yao.




Follow us on twitter Swahili World Planet  and Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, beauty, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news, life styles news and more

No comments:

Post a Comment