Friday, March 28, 2014

Bongo Movie Sio Chama Ni Kampuni Ya Watu Tisa Na Pia Sio Wanachama Wa Shirikisho La Filamu Tanzania: Simon Mwakifwamba


Simon Mwakifwamba
Rais wa Shirikisho La Filamu Tanzania(TAFF) Simon Mwakifwamba amewachana wasanii wanaounda kundi la Bongo movie kuwa hawajitambui na ndiyo maana wanafikiri usataa uko juu ya sheria. Mwakifwamba amesema kuwa wengi wanafikiri Bongo movie ni chama wakati ni kampuni ya watu tisa na wala sio wanachama wa shirikisho la filamu Tanzania kitu ambacho wengi wanashangaa wasanii wa kundi hilo la Bongo movie. Akizungumza na Globalpublishers Mwakifwamba ambaye pia ni muigizaji wa muda mrefu na pia Director wa filamu katika tasnia ya filamu Swahiliwood alisema...


“Bifu la nini? Mimi ni baba, wao ni watoto. Kwanza sikia... wale siyo wanachama wangu. Nawashauri wajiunge kwenye vyama vyangu ili niwatambue kama sehemu ya shirikisho.
“Unajua wale wanaongozwa na ustaa. Wanaamini ustaa upo juu ya sheria, siyo kweli. Mimi naamini katika uelewa na uwezo.
Isitoshe mtu wa kwanza aliyetoa wazo la Bongo Muvi ni mimi.
“Nakumbuka nilikuwa mimi, Dude (Kulwa Kikumba), William na Ruge Mutahaba, tukaunda Bongo Muvi ili tucheze mechi na Bongo Fleva kwa ajili ya kuchangisha fedha za waathirika wa mabomu ya Gongo la Mboto.
“Tulifanikiwa sana. Hapo sasa walafi wachache wakalazimisha wasanii waende Mwanza wakacheze mechi nyingine ili wapate fedha, nikakataa hilo wazo, ndiyo mwanzo wa kutengana nao. Niwaambie tu Watanzania, chombo mama cha wasanii wa filamu nchini ni TAFF, si vinginevyo.
“Kwanza Bongo Muvi si chama kama wengi wanavyofikiri, ni kampuni na ina wamiliki wake tisa, hao wengine wanafuata mkumbo kwa sababu hawajitambui. Kama wanabisha, waonyeshe usajili wao wa Basata, maana chombo pekee kinachosajili kazi za wasanii ni Basata.”



Follow us on twitter Swahili World Planet  and Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, beauty, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news, life styles news and more

No comments:

Post a Comment