Dar es Salaam. Imezoeleka kuwa
klabu za usiku zimekuwa zikitumika kwa mambo ya starehe huku viongozi wa
dini wakizichukulia kama maeneo hatari kwa waumini wao.
Tofauti na maeneo mengine ya
starehe, klabu za usiku huwa na kumbi za muziki zenye taa za kumweka za
rangi mbalimbali huku giza likitawala. Wakati huo huo muziku hupigwa kwa
sauti ya juu.
Mbali na muziki, klabu hizo
husheheni vileo vya kila aina huku watu wakiruhusiwa kuingia na mavazi
yoyote wakiwemo wale wanaopenda kuvaa nuzu uchi.
Hata hivyo kwa watumishi wengine wa Mungu, klabu sasa ndiyo pamekuwa mahali pa kuvunia waumini.
Mchungaji Harris Kapiga wa kanisa
la Nchi ya Ahadi lililoko Sinza Kamanyola, ameamua kuanzisha klabu ya
usiku kama zilivyo klabu nyingine za starehe.
Klabu hiyo iliyozinduliwa hivi
karibuni maeneo ya Mbezi Tangibovu katika hoteli inayoitwa MakHotel,
imeonekana kuvutia vijana wengi ambao walionekana wakifurahia mandhari
na muziki uliokuwa ukipigwa ndani yake.
Tofauti na klabu nyinginezo,
Mchungaji Kapiga anasema kutakuwa na udhibiti wa vishawishi vya dhambi
ikiwa pamoja na ulevi, mavazi yasiyo na staha na aina ya muziki
unaopigwa.
Anasema tangu alipoanzisha wazo hilo, watu wengi hasa wachungaji walikuwa na wasiwasi kuhusu vishawishi hivyo.
“Tangu nimeanza wazo langu hili
nimekumbana na vikwazo vingi. Imeshtua watu wengi, japo wengi
wamelikubali na kuna baadhi hawakubali ila hawawezi kusema wazi,”
anasema na kuongeza:
“Wengine wanajiuliza nitawezaje
kudhibiti vipi hali ya klabu kwa sababu maeneo haya kunakuwa na anasa,
ulevi na masuala ya mavazi watu watavaaje, na mimi nawajibu.”
“Mtu akija hapa na mavazi mabaya
hataingia, tutakuwa makini sana katika hili. Mtu avae nguo yenye staha,
siyo mtu aje nusu uchi, tutamtoa kwa nia njema tu. Hata mtu aliyelewa
tutamtoa labda tusimgundue.”
Kwa
nini ameanzisha klabu ya usiku? Mchungaji Kapiga anasema alianza kupata
wazo hilo siku alipokuwa kwenye sherehe za kuadhimisha kuzaliwa kwa
Clouds Media ambako pia ameajiriwa kama mtangazaji
credit: teenzchoice
No comments:
Post a Comment