Thursday, January 2, 2014

NAKERWA SANA NA VYANGUDOA WANAOJIITA WASANII: MARIAM ISMAIL

Mariam Ismail ambaye ni actress aliyejipatia umaarufu katika tasnia ya filamu Swahiliwood kutokana na kipaji chake bila kuwa na skendo yoyote kama baadhi ya wasanii ameamua kuwachana baadhi ya wasanii wanaofanya vitendo vya kifuska kwa kujiuza akisema ni kinyume na miiko ya sanaa. Mariam alisema kuwa badala ya wasanii kuigiza kwa ustadi mkubwa nafasi wanazopangiwa kucheza wao huendekeza skendo ili kujipatia umaarufu na kufanya vitendo vya uchangudoa kwa kuuza miili yao na kuichafua tasnia nzima. Akizungumza na gazeti la Dimba star huyo wa filamu za Omega Confusion, Return Of Omega, Best Man, Sobbing Sound na Apple alisema.......

"Hakuna kitu ninachokichukia kama kuuza mwili wangu kisa kusaka umaarufu, ndiyo maana nakerwa na wasanii wanaofanya hivyo kwani wanapaswa kucheza kwa umakini sehemu wanazopangiwa kucheza kama nilivyofanya mimi katika filamu ya The Return Of Omega ambayo kwasasa inafanya vizuri sokoni"

Mariam alisema kuwa filamu ya The Returm of Omega imezidi kumuongezea mashabiki kutokana na kucheza kwa ustadi mkubwa.

                                                      Mariam Ismail

Follow us on twitter Swahili World Planet  and Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, beauty, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news.

No comments:

Post a Comment