Thursday, January 2, 2014

MUIGIZAJI SABBY ANGEL ANUSURIKA KATIKA AJALI NCHINI KENYA. ADAI NI HUSDA ZA WATU.

Muigizaji wa filamu anayekuja juu Swahiliwood Salma Tamim maarufu kama Sabby Angel amenusurika katika ajali leo hii huko Nairobi nchini Kenya wakati akiwa katika mishemishe zake baada ya kukoswa koswa na gari lililporamia duka moja. Sabby alinusurika kwa kuvutwa haraka na msamaria mwema kutoka upande wa gari hilo lililokuwa limeacha barabara wakati akiwa katika duka la nguo la Kays LTD. Sabby akichonga na Swahiliworldplanet alisema kuwa hiyo ni husda tu kwani siku za hivi karibuni amekuwa akiandamwa na baadhi ya wasanii wenzake bila kujua sababu. "nimeshtuka na kuchukia sababu ni husda tu, hivi karibuni nimekuwa nikiandamwa na baadhi ya wasanii, wananiandama kwa maneno"

Star huyo wa filamu za Hard Price, Nimekubali Kuolewa na Moto wa Radi ambazo zitatoka muda si mrefu kuanzia sasa aliendelea kwa kusema kuwa atafanya kisomo  cha Maulid na kutoa sadaka ili Mungu amkinge na maadui wa husda "Nitafanya kisomo cha maulidi na nitoe sadaka kumuomba Mungu anikinge na maadui na husuda". Angalia picha za tukio hilo...............

Sabby alivyokuwa leo kabla ya kunusurika katika tukio hilo

Follow us on twitter Swahili World Planet  and Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, beauty, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news.

No comments:

Post a Comment