Thursday, January 9, 2014

ALICHOKISEMA ZAGAMBA JUNIOR KUHUSU TASNIA YA FILAMU NCHINI.

Zagamba Junior ni mwanafunzi anayesomea mambo ya filamu chuo kikuu cha Dodoma(University Of Dodoma) na pia mdau mkubwa wa tasnia ya filamu nchini ambapo mara nyingi huwa posts zake kuhusu filamu hunivutia na hii aliyoweka leo ni mojawapo iliyonivutia kwani ina points nzuri. Soma hapo chini..........

"Kiukweli elimu ya Film Nchini kwetu ni elimu ya darasani tu namaanisha haija balansi nadharia na vitendo.asilimia kubwa ni ya nadharia. Katika Tasnia ya FILM kuna Upungufu wa wataalamu walio bobea na hata hao wachache hawapati nafasi na hata wakipata nafasi hawapati vifaa vinavyo kidhi.Tatizo kubwa linalo wasibu wasomi wengi wanaotoka vyuoni ni kuwa hawana uzoefu, wengi hujifunzia majaribio wakiwa kazini hii ni kutokana na ufinyu wa vifaa vyuoni, wengi wanaelimu ya makaratasi. Wenye uzoefu ni wale wasio na elimu So kipi cha kufanya ili kupiga hatua katika tasnia ya film Tanzania.Kikubwa ni ushirikiano kuunganisha elimu ya mtaani ambayo inafaa kwa mazingira yetu na elimu ya darasani ili kuongeza kiwango na maboresho zaidi.

Changamoto tulio nayo ni kuwepo kwa migogoro /ama mikwaruzano ya chinichini kati ya wataalamu wenye elimu na wasio na elimu. Kila mmoja anataka aonekane Bora kuliko mwenzake, mmoja anajivunia ukongwe na uzoefu mwingine anajivunia elimu na ujuzi. Hapo ndipo inapotokea kitu Dharau na migogoro.Na sehemu yoyote yenye migogoro hakuna maendeleo kamwe.Heshima, uwajibikaji, ushirikiano na upendo ndio nguzo ya Maendeleo katika sanaa Tuondoe tofauti zetu za elimu, majina na utabaka.Tunapo ingia kazini hivyo vyote tuwekaepembeni tupige kazi kwanza mengine Baadae. Tasnia ni ngumu elimu peke yake wala majina peke yake hayawezi kufanya lolote.Tasnia inabadilika hakuna aliyezaliwa nayo pasipo ushirikiano unapotea dakika chache tu na unasahaulika na kubaki jina kavu. Kama Ukitaka kuona uhondo wa ngoma ingia ucheze"

                                                          Zagamba Junior



Follow us on twitter Swahili World Planet  and Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, beauty, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news, life styles news and more.

No comments:

Post a Comment