Monday, December 16, 2013

SIWEZI KUFUMANIWA NA MTU KAMA YOUNG D: LULU

Lulu
Mwishoni mwa wiki iliyopita mitandao mingi nchini ilikuwa na habari ya star wa filamu Swahiliwood Elizabeth Michael(Lulu) kufumwa na askari wa doria maeneo ya Mbezi Beach akifanya mapenzi ndani ya gari na msanii wa Bongofleva Young D. Baada ya habari hiyo wawili hao wamefunguka kupitia Globalpublishers
wa kwanza kutafutwa alikuwa Young D na alisema "Siyo kweli kabisa, isitoshe nina kama mwezi mzima sijaonana na huyo Lulu, huku ni kutaka kuchafuliana majina tu" alisema Young D.
 
Habari zinadai kuwa licha ya Young Dee kukanusha kuwa hajaonana na Lulu kwa muda mrefu, siku ya tukio walikuwa pamoja ingawa hawakutaka kuonekana na mtu yeyote.

Kwa upande wa Lulu alipotafutwa, alifunguka: "Kweli nimesikia ishu kama hiyo ila kinachonishangaza na kunisikitisha ni kwamba siku hiyo ya tukio inayotajwa mimi nilikuwa nyumbani na siku nzima sikutoka kwenda popote, hata hiyo Mbezi iliyotajwa mimi siielewi kabisa, hata lile gari mimi sina gari la aina hiyo wala sijawahi hata kulipanda gari hilo na huyo Young Dee nina muda mrefu sana sijaonana naye"

"Usiku wa kuamkia leo nilimpigia mtangazaji mmoja ambaye aliirusha habari hiyo redioni, nikataka kujua ameipata wapi habari hiyo? Akanijibu kwamba amepata tetesi tu. Sasa kama ni tetesi kwa nini asichunguze kabla hajanichafulia jina?"

"Pia alisema kuna askari wa doria walitukamata, nikamtaka anipeleke hicho kituo cha polisi tulikopelekwa ili tuthibitishe kama ni kweli maana ishu hii inanichafua mimi na familia yangu, akashindwa kufanya hivyo."
"Yaani naomba ieleweke kuwa sijafumaniwa na siwezi kufumaniwa na mtu kama Young Dee maana  kwanza hata sijawahi kukutana naye hivi karibuni, sipendi kuchafuliwa na haya yote namuachia Mungu atawajibu wote wanaonizushia," alisema Lulu.

Young D

Follow us on twitter Swahili World Planet  and Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, beauty, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news.

No comments:

Post a Comment