Saturday, November 30, 2013

NISHER AMTIBUA ZUHURA GORA BAADA YA KUDAIWA KUJILINGANISHA KIKAZI NA ADAM JUMA.

Zuhura Gora
Zuhura Gora ambaye ni model na actress nchini amemshukia Nisher ambaye ni director na producer chipukizi wa video za muziki wa Bongofleva baada ya kudaiwa kujilinganisha kiubora kwa kazi na Adam Juma ambaye alileta mabadiliko ya kutengeneza video bora za muziki wa Bongofleva nchini. Issue hiyo iliwafanya Nisher na Adam Juma waanze kutupiana maneno kwenye mitandao ya kijamii na blogs kuanza kuandika habari hizo. lakini Nisher ambaye pia ana kazi nzuri licha ya uchanga wake kwenye fani hiyo alikaririwa na Bongo5 akisema kuwa watu walimuelewa vibaya na wala hakumaanisha watu walichotafsiri ingawa wengine walisema sio kweli anajibaraguza tu ila alimaanisha hivyo hivyo.

Kupitia mtandao mmoja wa kijamii Zuhura ambaye ni mpenzi wa Hemedy, video model wa wimbo wa Kamili Gado wa Professor J na pia anatarajiwa kuonekana kwenye tamthilia ya Siri Ya Mtungi season 2 aliandika " Hey Nisher o vyovyotee unavyojiita stop kum-diss my boss coz humfikii hata theluthii hujishtukiii kujifananisha na Adam Juma, nyooo mpxiiiieeww jipangeee usiwe mburulaaa muoneee umeniboa for this haki ya Mungu walahi umenitibua"

                                              Adam Juma na Nisher

Follow us on twitter Swahili World Planet  and Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, beauty, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news.

No comments:

Post a Comment