Star wa filamu Swahiliwood Diana Kimaro ametamba kuwa hakuna muigizaji yeyote wa kike anayemtisha nchini kwa kuwa wengi wapo kawaida tu katika uigizaji na hawana ubunifu. Diana ambaye amatoa upinzani mkubwa kwa Lulu katika filamu ya Foolish Age na Family Disaster alisema kuwa kwasasa amerudi kwa kasi baada ya shule kumbana kidogo na anakuja na filamu mpya ya Kigodoro Kanitangaze ambayo amecheza kama mhusika mkuu na kutoa tahadhari kwa shoga yake Elizabeth Michael Lulu ambaye mara nyingi watu humfananisha nae kama mapacha baada ya kuigiza pamoja filamu kadhaa na kufanya vizuri.
Akizungumza na
Filamucentral Diana anayepatia sana akicheza scenes za kimcharuko alisema "Nilipokuwa shule nilijitenga na sanaa sasa nimerudi watasubiri kwa
upande wa wasanii wa kike wanaigiza kwa kiwango cha chini, au kwa
kutopewa nafasi wanazomudu kuna watu wanajua mimi na Lulu ni mapacha
lakini kwa filamu niliyoifanya hivi karibuni ya Kigodoro shoga yangu
atasubiri"
Tayari kuna filamu mpya za Diana zimetoka hivi karibuni na nyingine zinakuja akiwa na mastaa wenzake akiwemo Jacob Stephen(JB).
Diana Kimaro.......
Follow us on twitter Swahili World Planet and Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP
for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities,
features, beauty, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and
Nollywood news.
No comments:
Post a Comment