|
Nisha |
Actress maarufu nchini Salma Jabu(Nisha) anadaiwa kuwa mmoja wa mastaa wa kike wachapakazi wenye mafanikio huku akiwa hana mbwembe nyingi za kujionyesha sana kama baadhi ya mastaa wenzake walivyo full mbwembwe. kwasasa Nisha anafananishwa na star mwenzake Jenifer Kyaka(Odama) ambaye anafanya vizuri sokoni na filamu nyingi huku akiwa hana skendo yoyote ya kumchafua badala yake anahakikisha kampuni yake ya J-FILMS 4 LIFE inazidi kutanuka kila uchao kama ilivyo kwa Nisha na kampuni yake ya Nisha's Film Productions.
Miezi ya hivi karibuni Nisha amekuwa mbali na skendo huku akihakikisha anapiga kazi vizuri na kuzalisha filamu baada ya kufungua kampuni yake tofauti na kipindi cha nyuma ambapo skendo zake zilikuwa magazetini mara kwa mara. Filamu ambazo zimemuongezea umaarufu mwaka huu ni pamoja na Tikisa na Pusi na Paku ambazo amezitengeneza yeye mwenyewe. Juzi pia alifanya usaili kwa ajili ya kuwainua wasanii chipukizi kwa ajili ya kufanya kazi na kampuni yake ambapo usaili huo utaendelea wikiend hii.
Odama
Follow us on twitter Swahili World Planet and Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP
for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities,
features, beauty, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and
Nollywood news.
No comments:
Post a Comment