Pages

Thursday, September 19, 2013

JOHARI NA CHUCHU HANS WAFUNGUKA BAADA YA KUPIGANA KISA KIKIWA NI RAY.

Chuchu Hans
Juzi Swahiliworldplanet iliandika kuhusu mastaa wawili wakubwa wa filamu Swahiliwood Chuchu Hans na Johari  kupigana kisa kikidaiwa kuwa ni penzi la star mwenzao Vicent Kigosi(Ray) ingawa hatukuweza kuwapata kwa wakati ili wao kutoa maelezo yao wenyewe. Timbwili lilitokea ofisi ya Rj Company iliyopo Sinza Dar es salaam ambayo inamilikiwa na Ray na Johari. Inadaiwa kisa ni Chuchu kutamba kuwa amempokonya Johari bwana'ke ndiyo Johari akapata hasira na kufumuana makonde lakini Chuchu alizidiwa na kupiga mayowe ya kuomba msaada ndipo Ray aliyekuwa nje ya Ofisi aliwahi kuwaamulia. Chuchu alienda ofisi za Rj lakini Johari hakuwepo alikuwa hoteli jirani wanashuti filamu mpya na akapewa habari kuwa Chuchu yupo ofisini ndiyo akatia timu na kukinukisha. "Unajua kilichomshtua Ray ni kilio cha Chuchu aliyekuwa akiomba msaada baada ya kuzidiwa na Johari, Ilikuwa ni bonge la soo, watu walijaa sana, baadaye Ray alimtoa Johari nje huku akimfokea, unaambiwa Johari alikuwa akikimbia na Ray kumfukuza, jambo lililovutia watazamaji wa sinema hiyo ya bure" kilisema chanzo kimoja kikizungumza na Gpl

Alipoulizwa na Globalpublishers kuhusu sakata hilo Johari alisema "Ni kweli lakini nani amekuambia? Unajua kilichoniudhi mimi ni maneno machafu ya huyu dada (Chuchu) anavyotamba kwa watu kuwa amenipokonya mume, wakati hakuna ukweli juu ya hilo, nilishikwa na hasira sana ndiyo maana nikaamua kumpa somo kidogo, Inaniuma kwa sababu mimi na Ray tumetoka mbali sana hadi kuisimamisha RJ. Tulikuwa hatuna kitu kabisa tukaungaunga huku na kule hivyo Chuchu anapaswa kutambua hilo. Asitake kunikumbusha vitu vingi kwa sababu tuliteseka sana,” alisema Johari kwa uchungu

Johari alipoulizwa kama bado anakwenda Rj baada ya kisanga hicho alisema " Tangu ile ishu itokee sijaenda RJ kwa sababu Ray alinifukuza eti kisa Chuchu. Usiniulize muafaka wa hili jambo kwa sababu hadi sasa sina majibu ya moja kwa moja kuna vitu naviweka vizuri"

Chuchu Hans ambaye pia ameigiza baadhi ya filamu kutoka Rj alipoulizwa alisema " Aaah, jamani sina cha kusema juu ya hilo, nikiwa tayari nitawaambia, Kinachonishangaza kila Johari na Ray wakigombana huwa natajwa mimi. Yaani sijui hata haya mambo yanatokea wapi"

Ray nae alipoulizwa alisema " Sikia Brighton (mwandishi), hili jina nimelitafuta kwa miaka mingi. Nakuomba usiandike habari hiyo, sielewi chochote.
“Ugomvi wao siujui na wakigombana waache kunitaja, waeleze sababu zao za kugombana siyo kunitajataja mimi,” alisema Ray na hata alipoulizwa uhusiano wake na mastaa hao wa kike aliishia kujiumauma bila kutoa majibu ya kueleweka.

                                                                   Johari
Follow us on twitter Swahili World Planet  and Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, beauty, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news.

3 comments:

  1. Chuchu you are so beautiful bt a bitch, Ray ni Malaya tu kutoka na kila mwanamke

    ReplyDelete
  2. Ray kashadata kwa binti wa kitanga huyo mpaka amemsahau Johari. Halafu nyie mbona mnajiaibisha kugombea mwanaume wakati wamejaa telee khaa!

    ReplyDelete
  3. Johary dawa ni kumtandika Ray mpka ajiheshimu coz kujitoa kwake ni ngumu shauri mko shea au akupe chako uchape lapa..CHUCHU kimalaya tu anatoka nawatu wengi c ray peke yake anayejifanya kafika kwake..

    ReplyDelete