Pages

Friday, September 6, 2013

DRAMA ZA WEMA SEPETU ZAGONGA MWAMBA MBELE YA LULU.

Wema
Wema Sepetu anadaiwa kutaka kuitawala katika media shughuli nzima ya uzinduzi wa filamu ya Foolish Age ambayo Elizabeth Michael(Lulu) na Diana Kimaro ni moja wa waigizaji wakuu wa filamu hiyo. Uzinduzi wa filamu hiyo ulifanyika tarehe 30 mwezi wa 8 Mlimani City, Dar es salaam. Muigizaji mmoja wa kike maarufu ambaye alikuwepo ukumbini hapo siku ya uzinduzi huo akizungumza na Swahiliworldplanet alisema kuwa hakuona umuhimu wowote wa Wema kujichetua namna alivyofanya wakati shughuli ilikuwa ya Lulu, alisema kuwa kitendo cha kwenda kumpa pesa Mama Kanumba hakikuwa na maana pale mbele za watu bali kujichoresha kwenye media ili auze magazeti kama kawaida. " Wema nae haachi kujichetua kila siku, shughuli ni ya mwenzake lakini alitaka kila mtu ajue kuwa Wema yupo ukumbini, kama alikuwa na nia ya kumpa mama kanumba pesa si anagempa tu nyumbani kwake au anataka attention kila alipo."

Muigizaji huyo aliongeza kwa kusema kuwa Wema ni mtu wa kumwaga pesa huku akishindwa kutoa filamu yoyote mpaka sasa kupitia kampuni yake iliyozinduliwa kwa kishindo mwanzoni mwa mwaka huu wakati mwenzake Lulu akizindua filamu yake na tayari ipo sokoni kwasasa huku ile ya Wema ya Superstar iliyozinduliwa kwa gharama kubwa na kutangazwa sana haijulikani ilipo mpaka leo. " mpaka sasa Wema hajatoa filamu yoyote na hata ile tuliyohudhuria uzinduzi wake mwaka jana kwa kumleta Omotola sijui kamuuzia nani, ajipange kama mwenzake,  unajua Wema alitaka kuitawala ile event kupitia media kwa kumfunika Lulu lakini Lulu alifunika siwamjua Lulu tena, shosti yake Kajala pia hakujituliza kitini mbona mastaa wengine walikuwepo bila drama zozote!" alisema muigizaji huyo kwa sharti la kutotajwa jina lake akizungumza na Swahiliworldplanet.

Wema, Kajala na mama Kanumba katika uzinduzi wa filamu hiyo
Follow us on twitter Swahili World Planet and Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, beauty, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood new

1 comment:

  1. Kiukweli Wema ni m2 wa kupenda sifa kila sehemu anapokua.

    ReplyDelete