Pages

Tuesday, September 17, 2013

BATULI AMTUPIA SWALI LA KIMITEGO RAIS KIKWETE.

Star wa filamu Swahiliwood Yobnesh Yusuph(Batuli) ameuliza swali likionekana kama la kimitego kwa Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete kuwa, je ikitokea amehojiwa kuwa ni star gani wa filamu Tanzania anaweza kujivunia mpaka sasa atajibuje. Kupitia twitter Batuli aliandika "Natamani kujua mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete ikitokea amehojiwa hivi atajibu nini-"ni mcheza filamu gani wa kike/kiume unaeweza kujivunia Tz?"

Hii si mara ya kwanza kwa muigizaji huyo maarufu wa filamu kuelezea hisia zake au maoni yake kwa Rais Kikwete kwani huko nyuma aliwahi ku-tweet moja kwa moja kwa mkuu huyo wa nchi akimuomba alivunje BASATA na kuliunda upya kwa kuwa halina msaada mkubwa kwa wasanii wakiwemo wa filamu ambao bado kila siku kilio chao ni kuwa kazi zao zinakubalika ndani na nje ya nchi lakini serikali bado imelala katika kuchukua hatua za dhati ili wasanii wafaidike na kazi zao.

 Baadhi ya matatizo makubwa ambayo wasanii wanataka ufumbuzi au msaada kutoka serikalini ni kama vile kutokuwa na sheria za dhati au kali za kumlinda msanii, mikataba ya kinyonyaji kwa wasanii, kunyimwa location au kuwa ngumu kupata location kutoka taasisi za serikali kama vile kuigiza mahakamani, Vyuo vikuu nchini, Hospitali kubwa na maeneo mengineyo na matokeo yake baadhi ya filamu kukosa uhalisia sababu ikiwa serikali kutotilia maanani tasnia ya filamu nchini. Wasanii wengi nchini wana majina makubwa kazi zao zinakubalika lakini bado maisha yao hayaendani na ukubwa wa majina yao kwa kuwa vipato bado ni vidogo.

Rais kikwete atajivunia msanii gani kwakuwa wengine wanaishia kusifiwa kwenye media au na viongozi lakini maisha yao bado ni duni hayalingani na umaarufu wao. Mfano marehemu Kanumba ingawa alikuwa na mali kadhaa lakini zinadaiwa bado hazikulingana na umaarufu wake huku filamu zake bado zikiendelea kuuza mpaka leo. Hata hivyo habari mpya ni kuwa uongozi wa BASATA tayari umebadilika na baadhi ya viongozi wapya ni John Kitime, Eric Shigongo na Dr.Vicensia Shule ambao wote wanaelewa vizuri matatizo ya sanaa na wasanii nchini hivyo tunategemea mazuri kutoka kwao.

                                                             Batuli
Follow us on twitter Swahili World Planet  and Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, beauty, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news.

10 comments:

  1. Huyu star mzuri jamani mpaka anakera. Batuli keep it up. Samira

    ReplyDelete
  2. Nikiingia twitter naenjoy kusoma speech za Batuli

    ReplyDelete
  3. Cleopatra NAKUPENDA DA BATULI. MIMI JONAS

    ReplyDelete
  4. Mutoto ya nguvu usimtie majaribu rais wetu

    ReplyDelete
  5. LOVE U BATULI WANGU WEEK END ILIYOPITA NILIKUONA REGENCY LAKINI NILIKUOGOPA NILIONA UPO NA WATU WAZITO. KEEP IN TOUCH BATULI

    ReplyDelete
  6. She believed, she could so she did ila batuli mcute sana mwaaaah

    ReplyDelete
  7. Mnajipendekeza kwa Mheshimiwa Balozi haya Batuli usilewe sifa chapa kazi

    ReplyDelete
  8. I like your life style Batuli very cool and big name xoxo. Jamila

    ReplyDelete