Baby Madaha ambaye ni staa wa filamu Swahiliwood na mwanamuziki wa Bongofleva amesainishwa mkataba na kampuni ya Candy n' Candy records Label iliyopo Nairobi, Kenya. Madaha ameingia mkataba wa mil 50, amepewa gari la kutembelea aina ya AUD TT na kupangishiwa nyumba nzuri ya kuishi maeneo ya Kijitonyama, Dar es salaam. Akizungumza na bongomovies Joe Kariuki ambaye ndiye mmiliki wa label hiyo ambayo pia ilimsainisha Mr. Nice kutoka Tanzania alisema kuwa Baby Madaha anakubalika sana nchini Kenya na wanataka kumhamishia Nairobi, Kenya kwa muda wa mwaka mmoja ili wafanye kazi kwa ukaribu zaidi.
Baby Madaha pichani hapo chini anatarajiwa kuzindua video ya wimbo wake wa Summer Holiday ambao amefanya na label hiyo. Staa huyo amecheza filamu nyingi na mastaa wenzake ikiwemo ya Ray Of Hope ambayo ilitwaa tuzo ya Africa Magic Viewers Choice Awards 2013(AMVCA) katika kipengele cha filamu bora ya kiswahili.
All the best Madaha
Follow us on twitter Swahili World Planet and Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP
for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities,
features, beauty, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and
Nollywood new
.
No comments:
Post a Comment