Actress wa Swahiliwood Aisha Bui ambaye amecheza filamu nyingi ambazo kuna alizoigiza na marehemu Steven Kanumba amefunguka kuwa ameshangazwa na madai yaliyoenea kuwa amefungwa nchini Brazil baada ya kunaswa na unga. Aisha amesema kuwa yeye amemfuata mchumba'ke nchini Brazil na alipoondoka nchini Tanzania aliondoka kimya kimya maana alijua ni lazima watu watazusha mambo na kumpaka matope ya kumchafua. Akizungumza na
Globalpublishers Aisha aliyejaaliwa mvuto alisema "Jamani hayo madai ya kwamba mimi nimefungwa huku(Brazil) kwa kesi ya madawa ya kulevya hata mimi mwenyewe nayashangaa, nipo huku kwa mwezi wa nne sasa nimekuja kwa mchumba wangu. hizo taarifa za kwamba eti nimefungwa ni uzushi unaotengenezwa kwa nia ya kunichafua tu"
Star huyo wa filamu aliendelea kwa kusema kuwa "wakati naondoka Tanzania ilikuwa kimya kimya kwakuwa nilijua kuna baadhi ya watu watazusha mambo ya kunipaka matope na ndicho walichofanya. Naomba watanzania wajue niko huru kabisa naendelea na shughuli zangu kama kawaida, natarajia kurudi Bongo hivi karibuni"
Aisha Bui
Follow us on twitter Swahili World Planet and Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP
for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities,
features, beauty, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and
Nollywood news.
não se preocupe querida... Gentes falam muito.. Faça o que é boa para te não esculta balho deles
ReplyDelete