Pages

Friday, August 2, 2013

NANI KATI YA HAWA ATAFUNIKA KATIKA TASNIA YA FILAMU? NAJMA, SALHA ISRAEL OR SABBY ANGEL?

Hawa wote ni waigizaji wapya na warembo katika Swahili movies na wote wanakuja na filamu kutoka Rj Company ambayo ni moja ya kampuni za kutengeneza filamu ikiwa inamilikiwa na Vicent Kigosi(Ray) na Blandina Chagula(Johari). Wasome na waangalie hapo chini........................

1.Najma: Huyu pia ni mwanamuziki wa Bongofleva na aliwahi kudaiwa kuwa mapenzini na Mr.Blue na sasa ameingia katika tasnia ya filamu, anakuja akiwa katika filamu ya Fans Death akiwa na Vicent Kigosi(Ray) na Rammy Galis.

 2.Salha Israel: Huyu ni mshindi wa taji la Miss Tanzania 2011 na anakuja na filamu ya Bad Luck pia kutoka Rj na amecheza kama mmoja wa waigizaji wakuu akiwa na Yobnesh Yusuph(Batuli), Johari na Baba Haji.

3.Sabby Angel: Huyu ni mwanamuziki mpya wa Bongofleva na sasa ameingia kwenye tasnia ya filamu nchini anakuja na Filamu ya Hard Price akiwa na Vicent Kigosi(Ray). Pia anakuja na Dr.Cheni katika filamu ya Nimeamua Kuolewa na kuna nyingine anafanya na kampuni ya Pili Pili.

Baada ya kuwasoma na kuwaona hapo juu unadhani ni nani atafanya kweli na kutikisa kwenye tasnia ya filamu nchini kama actresses wengine wanaotamba sasa?. Pia baada ya filamu zao wote kutoka tutaziangalia hasa performances zao na acting skills kwa ujumla na tutakuletea hapa. Kwa maoni yako unadhani nani atafunika na kuwa star mkubwa wa filamu nchini?

Like our facebook page Swahili World Planet for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, fashions plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news.

No comments:

Post a Comment