Pages

Saturday, August 24, 2013

CYRILL KAMIKAZE AZUNGUMZIA NGOMA YAKE MPYA NA ISSUE YA KUTAFUTA MWANDISHI MZURI WA MASHAIRI ILI WAFANYE KAZI PAMOJA.

Baada ya kufanya poa sana katika ngoma ya Utamu Wa Chocolate aliyoshirikiana na Bob Junior ,hit maker wa ngoma hiyo Cyril Kamikaze wiki hii ameachia ngoma nyingine ambayo pia ni hit. Wimbo huo mpya unaitwa "Fumba Macho" na unafanya poa sana katika vituo mbalimbali vya radio kwa sasa kutokana na style ya wimbo wenyewe pamoja na msanii aliyeshirikina nae ambaye ni Dullayo. Akifanya mahojiano na Patrick Derrick Mwankale mtangazaji wa kipindi cha Strengo Saturday kinachorushwa kila jumamosi kupitia radio Victoria fm ya Musoma, Mara Cyril amesema fumba macho ni ngoma nzuri sana ambayo ina mabadiliko makubwa sana tangu aanze kuimba. Hii ni kwasababu ameshirikina na msanii Dullayo ambaye pia anamkubali sana katika muziki anaofanya. Amesema imekuwa tofauti pia na ngoma yake ya Utamu Wa Chocolate kwasababu hata maudhui ya ngoma yenyewe pamoja na ujumbe uliopo kidogo ni tofauti.


 Aidha Cyrill kamikaze amesema pia anatafuta mtu ambaye anaweza kuandika nyimbo tofauti tofauti ili amuajiri na kumlipa katika ishu hiyo kutokana na yeye kubanwa na majukumu ya kikazi kiasi cha kushindwa kuandika au kuingia studio mara kwa mara .
Akijibu swali la mtangazaji wa kipindi hicho aliyetaka kujua kuhusiana na suala lake la utafutaji wa mtu wa kuandika mistari ambapo alipost kupitia ukurasa wake wa facebook kuwa natafuta mtu wa namna hiyo, Cyril alisema, "unajua sisi watanzania huwa wakati mwingine tunafanya kazi nyingi mno kupitiliza, na hiyo ishu ni kweli natafuta na bado nahitaji mtu wa kuniandikia nyimbo ambaye nitamlipa na kumuajiri kabisa ,ila awe mwandishi mzuri anayesoma mazingira na anayekwenda na wakati na awe anaandika kila aina ya nyimbo. nafanya hivyo maana hivi sasa nipo busy sana na majukumu ya kiofisi kaka. na bado muziki naupenda sana ndiyo maana sitaki kuupoteza kabisa , kwahiyo kama atatokea mtu ambaye yupo willing kufanya hivyo tunaweza fanya biashar" alimalizia Cyrill

 Like our facebook pages Swahili World Planet Planet and Bongomovies SWP for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news

No comments:

Post a Comment