Pages

Wednesday, July 31, 2013

SINA TATIZO NA JINI KABULA: ISABELA MPANDA.

Isabela Mpanda ambaye ni mwanamuziki wa bongofleva na pia muigizaji wa filamu amesema kuwa yeye hana tatizo na star mwenzake Jini Kabula ambaye waliripotiwa kugombana hivi karibuni na Bella kudaiwa kumtupia vitu nje Kabila. Bella alisema ni kweli aligombana na Jini Kabula ambaye pia ni star wa filamu na music katika kundi la Scorpion Girls lakini alisema hakumtupia vitu nje kwani Kabula anaishi kwake na familia yake. Ukiachilia mbali hayo Bella amesema ameamua kutoa single na wimbo wa "Jikubali Mwenyewe" ikiwa kama sehemu ya kujiimarisha kimuziki lakini bado yupo Scorpion Girls ambalo linaundwa na yeye, Kabula, Jackline Pentezel, Aunt Lulu na Husna Id Sajent. Akizungumza na Hatua Tatu ya Times fm Isabela aliongeza kwa kusema kuwa Luteni Kalama ndiye meneja wake ambaye pia ni mwanamuziki na mchumba wake na mipango yao ni kuoana na kuwa na familia.

Like our facebook page Swahili World Planet for more updates about Swahili movies' latest news, gossip, celebrities, features, fashions plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news

No comments:

Post a Comment