Muigizaji mmoja maarufu nchini ambaye kwasasa yupo nje ya nchi amesema kuwa katika safari yake hiyo nje ya nchi moja ya vitu anavyofanya ni kushawishi na kuzungumza na baadhi ya kampuni za nje ili kuweza kuwekeza nchini katika tasnia ya filamu hasa katika usambazaji ambao kwasasa unadaiwa kuwepo kwa kuangalia jina la star aliyepo ndani ya filamu husika au ukaribu wa msanii na msambazaji pasipo kuangalia ubora wa kazi zikiwemo kutoka kwa waandaaji na wasanii chipukizi. "nimeshaongea na kampuni moja wanataka kufanya hivyo kwa kusambaza nchi tofauti pamoja na Tanzania na ndiyo wanataka kuanza kwa hiyo naona itakuwa vizuri ngoja tuone" alisema msanii huyo akiongea na Swahiliworldplanet.
Kuhusu wasanii wa Tanzania kuanza kusambaza kazi zao kupitia katika mitandao kama baadhi ya nchi zilizoendelea msanii huyo alisema " kuuza net pia bongo imeanza wanafanya steps nasikia lakini bado itakuwa faidia yao siyo ya wasanii kama msanii unamuuzia kazi nzima huwezi kuhusika kwenye hayo mauzo"
Kwasasa bado kuna kampuni chache za kusambaza kazi za wasanii nchini na pia inadaiwa kuna msambazaji mmoja anawafanyia wenzake hujuma ili abaki yeye pekee katika kusambaza kazi za wasanii.
Uwepo wa kampuni nyingi za usambazaji utachochea ushindani katika kusambaza kazi za wasanii na hata malipo yao kuongezeka. Hii ni kwasababu licha ya filamu za kiswahili kupendwa nchi mbalimbali lakini bado zinashindwa kufika huko hivyo wasambazaji wengine wakijitokeza ni rahisi kufika mbali na soko kukua maradufu na wasanii pia kufaidika katika mapato, na hili litakuwa na tija iwapo wasanii hawatauza haki zao zote kwa wasambazaji kupitia mikataba ya kinyonyaji, sheria pia zinatakiwa kuwekwa ili kumlinda mtengenezaji wa kazi husika katika kufaidika na kazi zake bila kusahau elimu kuhusu tasnia ya filamu.
Baadhi ya wasanii wa filamu nchini
No comments:
Post a Comment