Pages

Tuesday, July 30, 2013

IRENE UWOYA AJA NA KIPINDI CHA TV KWA AJILI YA KUTENGENEZA NYUMBA ZA WATU.

Irene Uwoya ambaye ni muigizaji maarufu Swahiliwood anakuja na kipindi chake kipya cha Tv kwa ajili ya kutengeneza na kukarabati  nyumba mbalimbali za watu atakazotembelea. Kipindi hicho kitarushwa kupitia Clouds Tv na tayari actress huyo ameanza kushoot kipindi hicho kama anavyoonekana pichani hapo chini. Kupitia akaunti yake ya Instagram Uwoya aliwaomba watu wamsapoti kwa kuandika "Clouds Tv.......kipindi changu kipya kinahusu nyumba, natengeneza na kukarabati nyumba ....please nipeni sapoti ili kuwasaidia watanzania wenzetu". Irene Uwoya ni muigizaji mwingine aliyeamua kugeukia vipindi vya Tv pia ukiachilia mbali kuigiza filamu wengine ni Rose Ndauka na Wema Sepetu ambaye show yake kuhusu maisha yake halisi pia itarushwa Clouds Tv kuanzia mwishoni mwa mwezi wa nane mwaka huu hivyo kaa mkao wa kula katika Tv yako.

Like our facebook page Swahili World Planet for more updates about Swahili movies' latest news, gossip, celebrities, features, fashions plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news


No comments:

Post a Comment