Pages

Tuesday, July 30, 2013

INTERVIEW: AMANDA POSHY AZUNGUMZIA KAZI ZAKE ZA FILAMU NA KUMWAGANA NA BWANA MISOSI.

Amanda Poshy ni muigizaji wa siku nyingi ambaye anafanya vizuri kwa sasa katika tasnia ya filamu nchini huku akiwa ameigiza filamu mbalimbali na mastaa wenzake wengi. Swahiliworldplanet ilipata nafasi ya kumuuliza machache muigizaji huyo aliyejaaliwa mvuto na kipaji cha kuigiza.  Hivyo ili kujua mengi zaidi kutoka kwa Amanda endelea kusoma  interview hiyo hapo chini............................


SWP: Kuna kipindi ulipumzika kidogo katika kazi zako za filamu lakini hivi umerudi katika game, je mashabiki wako na waandaaji wa filamu wamekupokeaji kwa ujumla?

AMANDA: 
Kipindi nimepumzika nashukuru mashabiki wangu walikuwa wanajaribu sana kuniomba nirudi kwenye game na hii inaonyesha ni jinsi gani wana upendo na mimi hivyo bila kubisha nikarudi kwa ajili yao ili kuwaonyesha ni kiasi gani. Nashukuru sana napokea maoni ya wengi wakionyesha ni jinsi gani wamefurahi na mimi nazidi kuwaahidi watazidi kufurahi zaidi ya mwanzo. Ningependa kumalizia kwa kusema kuwa nawapenda sana mashabiki wangu.


SWP: Katika moja ya filamu zako zilizotoka hivi karibuni ni Nyumba 4 ukiwa na king Majuto na performance yako katika filamu hiyo ni nzuri, je unazungumziaje kufanya kazi pamoja King Majuto?
AMANDA:  Mmmmh....kwanza toka zamani nilikuwa na ndoto za kufanya kazi na Mzee Majuto na nashukuru Mungu nilifanikiwa hilo....nafurahi sana na hasa nikiwa naiangalia ile movie huwa kweli naona naweza.
SWP:  Kwahiyo bado ungependa kufanya kazi zaidi na King Majuto kuliko wasanii wa kiume wa rika lako?
AMANDA:  Napenda kufanya kazi na msanii yeyote because wote tupo katika fani moja na wote ni ndugu hivyo hata Mzee Majuto akihitaji kufanya kazi na mimi tena basi nipo tayari.
SWP: Ni kweli umeachana na Bwana Misosi?
AMANDA:  Ni kweli mimi na Bwana Misosi tuliachana muda mrefu tu na hatukuwa tukihitaji kuweka wazi lakini imenibidi kwasababu mashabiki wangu wengi walikuwa wanasumbua kutaka kujua uhusiano wetu upo au umekufa...ni kweli tumeachana. 

SWP: Lakini kutokana na alivyonukuliwa na media inaonyesha Bwana misosi hakutarajia media zijue kuwa mmeachana na inaonyesha kama bado anakupenda ila wewe hutaki?
AMANDA:  Kwa upande wake siwezi kumsemea moyo wake ila kwa upande wangu sipo tayari na wala sifikirii kurudiana nae....tumebaki marafiki wa kawaida tu.
SWP:  Sasa hupati usumbufu wowote kutoka kwa wanaume ukifikiria wewe ni mwanamke mrembo, uliyejaaliwa mvuto na maarufu pia?
AMANDA:  Ha ha ha haaa hiyo ni kawaida ila najiheshimu na naheshimu watu wote na kikubwa ninaye mtu wangu ambae tunaheshimiana sana.
SWP;  Ni muigizaji gani wa kike nchini unakubali sana kazi au kipaji chake na kwanini yeye?
AMANDA:  Namkubali sana Riyama Ally..yupo makini sana na kazi na anajua nini anafanya.
SWP: Wewe ni mmoja wa mastaa wachache wa filamu ambao huwa unajumuika na mashabiki wako moja kwa moja kupitia mitandao ya kijamii(social networks) kama vile Facebook na hata kuelezea hisia zako juu ya kitu flani wakati mwingine, hivyo unafikiri mastaa wengine ni muhimu kuwa karibu na mashabiki wao kama unavyofanya wewe kupitia social networks?
AMANDA:  Mimi binafsi napenda sana kuwa karibu na mashabiki wangu kwasababu nakuwa najua kwa urahisi nini wanapenda na nini wanachukia. Pia mara nyingi wengi wao huwa wananipa ushauri na naupokea kwa mikono miwili hivyo nawashauri wasanii wenzangu wawe karibu na mashabiki sababu kuna faida............maringo hayasaidii.
SWP:  Kwasasa una-shoot filamu gani na labda nyingine ambazo zimeshakamilika zinatarajiwa kuingia sokoni muda si mrefu?
AMANDA:  Kwa mwezi huu wa Ramadhani niligoma kupokea kazi yoyote hivyo mpaka mwezi ukiisha natakiwa kuingia location ku-shoot movie mpya pia nitaizungumzia nikianza. Lost Future na Panga La Moto zimeshakamilika na nina imani zitakuwa ni filamu bora na zitakazopendwa sana na mashabiki.
SWP:  Ni kitu gani huwa kinakukera katika tasnia ya filamu na ungependa kisiwepo?
AMANDA:  Sipendi wasanii wanavyobaguana hilo ndio kubwa linalonikera, wasanii tupendane kwa sababu wote tupo katika fani moja... i mean kazi moja so tupendane because wote ni ndugu.

Like our facebook page Swahili World Planet for more updates about Swahili movies' latest news, gossip, celebrities, features, fashions plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news
                                       xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

No comments:

Post a Comment