Pages

Monday, May 6, 2013

TUNA MENGI YA KUJIFUNZA KWA BOLLYWOOD KUADHIMISHA MIAKA 100.

Bollywood au kwa jina lingine filamu za kihindi zinaadhimisha miaka 100 tangu ilipotengenezwa filamu ya kwanza kabisa mwaka 1913 iliyoitwa "Raja Harishchandra". Mpaka kufikia ilipo sasa kwa kuwa namba moja duniani kwa uzalishaji wa filamu huku ikichuana sana kwa ubora wa filamu na mauzo na Holyywood imepitia katika matatizo mengi na bado inaendelea kujiboresha kila siku ili izidi kusonga mbele na kutamba. Watengenezaji wa kitanzania bado tuna safari ndefu kama walivyoanza wenzetu na pia tuna mengi ya kujifunza kutoka kwao ili kusonga mbele zaidi na kuwa na mawazo ya kimapinduzi zaidi. Ni wazi kuwa wapo waigizaji, waongozaji na watengeneza filamu wa Tanzania waliopata inspirations kutoka kwa filamu na waigizaji wa Bollywoood mfano mzuri ukiwa Jacob Stephen(Jb) ambaye alishawahi kukiri kumhusudu sana Amitabh Bachchan. Tuna mengi ya kujifunza kutoka india kama baadhi ya haya hapa...............

1. kwanza kabisa kutukuza mila na tamaduni zetu kupitia filamu zetu za kiswahili bila kuiga uzungu usio na tija. India imekuwa ikitumia Kihindi katika filamu zake na hata majina ya filamu zake asilimia 99% ni ya kihindi na siyo kizungu huku bado ikifanikiwa sana katika mauzo ya filamu hizo. Sanaa ni ubunifu na siyo lugha au kiingereza. Mfano zipo filamu kibao zilizotengenezwa kwa kiingereza hata kutoka Hollywood kwenyewe lakini zinaangukia pua mbele ya film critics wa huko huko Hollywood huku wakizipa alama za juu filamu kutoka Bollywood. hata sokoni filamu za kizungu nyingine hufanya vibaya huku za Bollywood zikitamba katika soko la nchi moja zinakouzwa.

2.Kutukuza mila na tamaduni zetu kupitia mavazi yetu ya kitanzania na mila zetu kwa ujumla kama vile za kimasai,kihadzabe, kinyakyusa, kisambaa na mila nyingine kama inavyofanya Bollywood kwa kutunza mila za jamii yao vizazi na vizazi. Filamu zetu ni lazima zijikite katika kuonyesha maisha halisi ya kitanzania na kiafrika na siyo kuiga uzungu usio na maana.

3. Serikali yetu ya Tanzania inatakiwa kutoa kipaumbele katika suala la filamu kwa kusaidia kwa vitendo zaidi na sio maneno matupu yaliyojawa na siasa. india inasapoti sana filamu zao na kuna tuzo kadhaa za serikali zinazotolewa kwa wasanii kutokana na kazi zao kila mwaka.

4. Serikali ya Tanzania na vyuo vyetu vinatakiwa kuanzisha hapa hapa nchini vyuo vya filamu ili watu wasome hapa hapa nchini katika mazingira asilia na siyo kwenda kusoma ulaya na marekani kwa kuwa mfumo wa filamu zao na mitaala yao ni tofauti na jamii na mazingira ya kiafrika na kitanzania. Watu wengi wa filamu nchini india hawataki kwenda kusomea filamu nje ya india kwa kuwa filamu zao ni tofauti na za Hollywood na hata jamii zao. Vyuo vyao hujikita katika kusisitizia mazingira yao, mila na tamaduni zao katika filamu zao.

5. Kutoona kuwa tuzo za Hollywood ndiyo bora kuliko nyingine zozote duniani. India imekuwa haizipi sana kipaumbele tuzo za Hollywood kama vile Oscar kwa kuwa inajua kuwa hazipo kwa ajili ya kukuza filamu za kihindi bali filamu za Hollywood hasa za wazungu wenyewe kwa kuwa miaka kibao film critics wengi hasa wenye asili ya Africa wamekuwa wakilaumu tuzo za Oscar kupendelea filamu za watu weupe/wazungu na kupotezea za watu weusi wa huko huko Hollywood. Hivyo sisi kama watanzania tuwe na tuzo zetu na sio kuamini kupata tuzo marekani ndiyo mafanikio. Lazima tuwe na tuzo zetu huku za nje zikiwa kama ziada tu.

6. Kuigiza Hollywood. baadhi ya waigizaji wa Bollywood wamekuwa wakipewa offer za filamu Hollywood lakini wanazikataa kwa kuwa hazipo kwa ajili ya kuwainua bali kuwaangusha mfano Star mkubwa wa Bollywood mwenye heshima kubwa mpaka Hollywood anaweza kupewa role ya filamu kama supporting actor huku underground wa Hollywood mwenye uwezo mdogo akipewa nafasi kubwa hivyo hukataa offer hizo kwa kuwa kama ni pesa wao pia hulipwa vizuri lakini lengo lao ni kuendeleza tasnia yao na sio kuonekana wadogo mbele ya wazungu. Hivyo wengi huwa makini na offer za Hollywood kwa kuwa sio zote zina manufaa kwao na wakati huo huo baadhi ya mastaa wa Bollywood wakiwapiku kwa umaarufu na utajiri waigizaji wa Hollywood.

7. Vituo vya Tv , magazeti, websites na blogs za Tanzania ziwe na uzalendo zaidi katika filamu na wasanii wa Tanzania na siyo kuona fahari kuandika habari za wasanii wa Hollywood au wa nchi nyingine na kuwaponda wasanii wa nchini  kwa kuwa hata Hollywood walianza kama sisi huku media zao zikiongoza uzalendo ndiyo sisi huku Afrika na Tanzania tukawajua wacheza filamu wa Hollywood, hivyo media na blogs zetu zikiongoza kuandika habari za sanaa zetu hao wa Hollywood pia watatujua sisi. Asilimia 90% ya media za burudani inchini India hutoa kipaumbele kwa sanaa zao. kama filamu zao na series zao lakini hapa nchini bado series za nje na filamu za Hollywood na Nigeria zinapewa nafasi katika baadhi ya vituo kuliko za wazawa wa kitanzania.

8.Elimu ya filamu bado inapewa kipaumbele sana Bollywood katika vyuo vya nchini mwao wenyewe huku elimu hiyo ikienda sambamba na kufunza mila na tamaduni zao katika kucheza na uandishi wa nyimbo za mahadhi ya kwao. Waandishi wakifunzwa kuhusu uzalendo na kuyajua vizuri mazingira na jamii yao. Hili pia linatakiwa liwe kwetu na baadaye katika filamu zetu za kiswahili kutukuza mila na tamaduni za Tanzania.

Hayo ni baadhi tu ya mambo ya kujifunza kutoka Bollywood inapoazimisha miaka 100 ya sinema zao. sio kuwa wamekamilika kwa kila kitu bado pia wanajifunza kila siku. Hata Hollywood waliopo juu katika technolojia na mauzo hawako kamili asilimia zote kwa kuwa pia wanajifunza kila siku.

Shahrukh khan muigizaji maarufu wa Bollywood, mwaka 2011 gazeti la Los Angels Times la Hollywood lilimtaja kuwa ndiye star mkubwa wa filamu duniani mwenye mashabiki wengi zaidi akiwa mbele ya Will Smith na Brad Pitt. liliandika hivi "the world's biggest movie star." katika makala yake hiyo kuhusu Shahrukh Khan.


No comments:

Post a Comment